Faida za kulia

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kila kitu alivyokiweka mwenyeziMungu usikichukulie poa, kina faida lukuki. Kulia ni kutoa machozi kwa uchungu au kwa furaha. Kulia kunaweza kuambatana na kutoa sauti ya kilio au kulia kimyakimya bila kutoa sauti.

Binadadamu anapokuwa na maumivu, hasira, au maudhi tendo la kulia au kumsimulia mwingine kile kilichomsibu ni sehemu ya tiba kwake inayoimarisha afya yake ya akili na mwili, kwa taaluma ya afya ya akili tendo la kulia, kuongea au kuhadithia mtu mwingine jambo linalokusibu tunaita mental ventilation au mental catharsis. Mtu anapoumia, umizwa au kupata taarifa asiyoipenda ni vizuri sana akapatiwa nafasi na muda wa kulia au kulisimulia jambo kwa uhuru kabisa.

Mfano, kama umemuadhibu mtoto ni vizuri kwa afya yake umuache alie hadi anyamaze mwenyewe bila kumlazimisha anyamaze/asipige kelele/asiongee. Ukimyamazisha kwa nguvu asilie au asisimulie wengine au kuongea ataendelea kulia ndani kwa ndani japokuwa hatoi sauti au hasemi lakini hasira itaendelea kubaki ndani ya mwili wake. Athali za kilio kubakia ndani kwa ndani ni mbaya na kubwa sana kwa mliaji, mazingira na watu waliomzunguuka. Anaweza kupata magonjwa ya moyo na tumbo, sonona (depression) au mlipuko (aggressiveness) wa liwalo na liwe.... kupotea, kujiua, kuharibu mali au kuua watu wengine.

Kwenye familia, taasisi, kazini, na jamii fanyeni yafuatayo:

itisheni vikao vya mara kwa mara ili watu wasimulie/wawasilishe yote yanayowakera na kuwakwaza kwenye familia, taasisi, kazini na kwenye jamii wanamoishi.

Tafuteni muda wa kutosha wa kila mtu mwenye lalamiko kuliwasilisha

Waacheni watu wawe huru kuyataja na kuelezea malalamiko yao, wasikatishwekatishwe.

Kila anaelalamika aombwe kutoa suluhisho la jambo analolalamikia

Familia, taasisi, kazini na jamii ichukue malalamiko yooote na masuluhisho yote wayachambue na kuyatekeleza kwa kufuata umuhimu wake, rasilimali zilizoko na uwezo mwingine uliopo kwenye familia, taasisi, kazini na kwenye jamii husika.

Kupigana virungu na kulazimisha waliopigwa wasilie wala kusimulia iko siku atakosekana mshindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…