Faida za kununiana na mpenzi wako katika ndoa au mahusiano

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
Mapenzi Yana wigo mpana mno ambao mtu anapaswa kuangalia kwa jicho Pana na akili pembuzi kabla ya kuingia,

Namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina Cha maji kabla ya kuzama, Sasa basi, zifuatazo ni FAIDA Tano (5) utakazo zipata ukiwa umenuniana na mpenzi WAKO.....twende kazi!!!

1. HUSAIDIA KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
👉Si kila rafiki wa mpenzi WAKO ana nia nzuri na uhusiano wengi au anafurahia penzi lenu, mathalani labda ww ni msichana na pengine miongoni mwa rafiki zake Kuna mmoja au wawili ambao hutamani Sana kupata penzi lako.

2. KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
👉Katika kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi ALILONALO huyo mtu wako Juu YAKo, kwa mpenzi aliye na hisia za dhati kwako, ktk kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu.

3. HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO

👉Ni kweli usiopingika kuwa, ktk Hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu Fulani ktk jamii unayoishi ni vigumu Sana kujikuta umekwaruzana naye, hii ni kwasababu itakuwa hauingiliani naye ktk mizunguko, vivyo hivyo kwa wapenzi.

4. KUBAINI TABIA 'X' ZA MPENZI WAKO
👉Hiki kipindi kitakusaidia kubaini TABIA na mienendo mibaya ya mwenzi wako, hii ni kwa kuwa itakuwa mbali naye hivyo nae hujiona kuwa Yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani kila mtu Hana time na mwenzake.

5. KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
👉 Hapa nieleweke, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa KUTAFAKARI penzi lenu kwa ujumla.

Nini maoni yako?, Je kwako ni sawa KUNUNIANA na MPENZI WAKO?
 
inasaidia sana kua na muda mrefu sana wa kuinjoy na mchepuko, lakini pia kuanzisha mahusiano mengune serious zaidi bila kupoteza muda.

zaidi sana inatoa fursa ya kipekee sana ya kuoa au kuolewa na mtu mwingine kwa haraka na hatimae wewe ujulishwe tu kuheshimu ndoa ya watu huku ukiwa umeduwaa macho kwa mstuko na mshangao wa kama utani au huamini vile :pedroP:
 
Kama nimeelewa, unamaanisha akikununia unampotezea mazima??,
mmoja kati ya waliochuniana kwenye mahusiano anaweza kuchukua hatua au amuzi huo. Na kuna muungwana moja ametoa ushuhuda kabisa kwenye uzi wa leo leo humu jukwaani :pulpTRAVOLTA:
 
Mapenzi Yana wigo mpana mno ambao mtu anapaswa kuangalia kwa jicho Pana na akili pembuzi kabla ya kuingia,

Namaanisha kwamba ni lazima kuchunguza kina Cha maji kabla ya kuzama, Sasa basi, zifuatazo ni FAIDA Tano (5) utakazo zipata ukiwa umenuniana na mpenzi WAKO.....twende kazi!!!

1. HUSAIDIA KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
👉Si kila rafiki wa mpenzi WAKO ana nia nzuri na uhusiano wengi au anafurahia penzi lenu, mathalani labda ww ni msichana na pengine miongoni mwa rafiki zake Kuna mmoja au wawili ambao hutamani Sana kupata penzi lako.

2. KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
👉Katika kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi ALILONALO huyo mtu wako Juu YAKo, kwa mpenzi aliye na hisia za dhati kwako, ktk kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu.

3. HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO
👉Ni kweli usiopingika kuwa, ktk Hali ya kawaida, ukiwa mbali na mtu Fulani ktk jamii unayoishi ni vigumu Sana kujikuta umekwaruzana naye, hii ni kwasababu itakuwa hauingiliani naye ktk mizunguko, vivyo hivyo kwa wapenzi.

4. KUBAINI TABIA 'X' ZA MPENZI WAKO
👉Hiki kipindi kitakusaidia kubaini TABIA na mienendo mibaya ya mwenzi wako, hii ni kwa kuwa itakuwa mbali naye hivyo nae hujiona kuwa Yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani kila mtu Hana time na mwenzake.

5. KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
👉 Hapa nieleweke, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa KUTAFAKARI penzi lenu kwa ujumla.

Nini maoni yako?, Je kwako ni sawa KUNUNIANA na MPENZI WAKO?
Kumbe kuna faida!
 
Back
Top Bottom