Faida za majani ya mstafeli

ng'ombo

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
418
Reaction score
619
Katika somo hili tutaona umhimu au faida 12 za majani ya mti wa mstafeli katika afya.

• Juisi yake hutibu kansa haraka na kwa ufanisi zaidi
• Ina nguvu mara 10,000 zaidi ya tiba ya mionzi katika kuziua seli za kansa
• Hutibu maumivu ya nyuma ya mgongo/low back pain
• Ni tiba ya asili ya maumivu ya mishipa, yasage majani yake mpaka yalainike kabisa kisha paka taratibu eneo la mshipa lililo na maumivu mara 2 kwa siku
• Hutibu maumivu ya jongo/gout
• Hurekebisha usawa wa kiasi cha damu sukari mwilini
• Huongeza kinga ya mwili
• Hudhibiti ukuwaji wa bakteria, virusi, vijidudu nyemelezi na uvimbe
• Huongeza stamina ya mwili na kurahisisha kupona haraka unapokuwa mgonjwa
• Hutibu jipu na vivimbe
• Hukimbiza chawa

Utatumiaje majani ya mstafeli kama dawa? Tengeneza chai kutokana na majani freshi ya mstafeli na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi mmoja. Inashauriwa hiyo chai unywe nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni.

Kama hutaweza kupata majani freshi ya mti wa mstafeli unaweza kutumia majani makavu ya mti huu yaliyo katika mfumo wa unga kwenye maduka ya dawa za asili sehemu nyingi hapa Tanzania.
Kwenye hiyo chai ya majani ya mstafeli ndani yake weka vitu hivi pekee; maji ya chai, majani ya mstafeli na asali au sukari, usiongeze majani mengine ya chai humo.

Pia inashauriwa utengeneze chai ya kutosha kuitumia kutwa nzima yaani uchemshe vikombe vitatu kwa wakati mmoja na uinywe kikombe kimoja kutwa mara tatu.

Au angalia video yake hapa =>Faida za majani ya Stafeli - fadhilipaulo.com

Share post hii na jamaa zako wengine
 
akhasante sana naimai umesaidia wengi
 
Dah kumbe nimekaa na hazina ya maana,ngoja nianze kuyatumia
 
kaka mie nasumbuliwa sana na gesi tumboni, je ni majani gani yanaweza yakatibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…