Faida za massage katika kuboresha mifupa

Joined
Aug 18, 2016
Posts
47
Reaction score
26
Faida za Massage katika Mifupa

Massage ina faida nyingi katika kuboresha afya ya mifupa. Mifupa ni tishu muhimu sana katika miili yetu, kwani mifupa huunda kiunzi ambacho:-
i. Huupa mwili umbo lake.

ii. Kiunzi kikishirikiana na misuli hutoa msaada/nyenzo ya kuuwezesha mwili kuwa katika mikao mbalimbali na kuhimili uzito wote wa mwili.

iii. Pia kiunzi huhifadhi viungo vya ndani vya mwili kwa mfano ubongo umehifadhiwa vizuri katika fuvu/skull, Pia mbavu(ribcage) huhifadhi mapafu na moyo.

iv. Husaidia mjongeo. Kiunzi humwezesha kiumbe kutembea ikishrikiana na misuli ya mwili.

v. Uzalishaji wa seli za damu. Seli za damu huzalishwa kwa wingi katika uroto(ujiuji unaopatikana katikati ya mifupa). Seli za damu nyekundu husafirisha gesi za upumuaji yaani oksijeni na Kabonidaiyoksaidi na seli za damu nyeupe hutoa ulinzi katika mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Hivyo ni muhimu sana kuhakikisha mifupa yetu inabaki katika hali salama ili tuweze kuishi kwa afya njema bila matatizo yoyote.

Hivi ndivyo massage inavyoboresha afya ya mifupa
Massage inaboresha mzunguko wa damu na hivyo kusaidia mifupa kupata virutibisho vya kutosha ili ibaki imara.

Massage huchochea ufyonzwaji wa madini ya Kalsiam na Fosforas katika mifupa. Madini haya ni muhimu sana kwa afya ya mifupa na kukiwa na upungufu inaweza kupelekea Osteroporosis-Mifupa kuwa laini na kuvunjika hovyo hata kwa kugongwa kidogo tu.

Massage husaidia kuondoa maumivu ya viungo(joints) na uvimbe katika viungo.

Happiness Massage Servives
0715 343 161 | 0756 343 161
 

Attachments

  • FB_IMG_15118612750967509.jpg
    136.6 KB · Views: 61
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…