Faida za maziwa ya mama kwa mtoto mchanga anyonyae

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Maziwa ya mama yanafaida nyingi sana kwa mtoto anyonyae mfano yanamkinga na Maradhi mbalimbali kwani yana virutubisho vinavyompa mpa kinga mtoto(Immunity),yana joto linalotakiwa na mtoto,ni rahisi kumeng'enywa na utumbo wa mtoto,Yanakuza upendo kati ya mama na mtoto...nk
Kitaalamu mtoto anapozaliwa anatakiwa apate maziwa ya mama tu kwa muda wa miezi 6(exclussively breastfeeding) labda kama mama anamatatizo anaeza chagua njia mbadala(replacement/mixed) feeding
ila siku za karibuni WAMAMA WENGI HAWAPENDI KUWANYONYESHA WATOTO WAO ILE MIEZI 6 YA MWANZONI BILA KUWAPA VYAKULA VINGINE TENA WENGINE HATA ILE MIEZ 6 HAWAMALIZI YOTE MTOTO ANAACHISHWA KUNYOYA...JE tatizo lipo Wapi???
 
Kabla uzi haujafika mbali, Uzoefu wako wa akinamama hawapendi kunyonyesha umeutolea wapi?
 
Mfumo wa maisha unabana sana asee, sidhani kama kuna mama asiependa kunyonyesha
 
Mfumo wa maisha unabana sana asee, sidhani kama kuna mama asiependa kunyonyesha
umenena...ila mtoto naye ni muhimu sana apate haki zake za msingi utapata mtoto anamiezi mitatu mtoto tiyari yuko kwa mfanyakazi wa ndani mama kurudi ni jioni
 
umenena...ila mtoto naye ni muhimu sana apate haki zake za msingi utapata mtoto anamiezi mitatu mtoto tiyari yuko kwa mfanyakazi wa ndani mama kurudi ni jioni
Sasa utafanyaje ndugu uache kazi ili ukae na mtoto?? Mtoto ni wa muhimu sana lakini inakua hakuna namna inabidi kazi ifanywe na mtoto alelewe
 
Sasa utafanyaje ndugu uache kazi ili ukae na mtoto?? Mtoto ni wa muhimu sana lakini inakua hakuna namna inabidi kazi ifanywe na mtoto alelewe
Maana ni sera ya serikali/dunia nzima je kuna umuhimu wa serikali kuwapa maternity leave miez sita ili wamama waweze kutimiza iyo sera vizuri badala ya miezi mi3?
 
Maana ni sera ya serikali/dunia nzima je kuna umuhimu wa serikali kuwapa maternity leave miez sita ili wamama waweze kutimiza iyo sera vizuri badala ya miezi mi3?
Duh ndugu yangu miezi sita??? Haya tuassune hiyo ni kwa serikali, kazi za watu binafsi kuna mtu yupo tayari kazi ilale miezi sita????
 
Duh ndugu yangu miezi sita??? Haya tuassune hiyo ni kwa serikali, kazi za watu binafsi kuna mtu yupo tayari kazi ilale miezi sita????
Baasi kama ni ivyo baasi hakuna haja ya serikali kusisitiza hii sera?siku hizi utapata watoto wengi wako overweight(obese) kutokana na kulishwa vyakula bila mpangilio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…