Faida za mchaichai

Faida za mchaichai

Herbalist Mtaturu

Senior Member
Joined
Aug 17, 2023
Posts
156
Reaction score
237
FAIDA ZA MCHAICHAI (LEMONGRASS)

Huu Mmea ni Mmea Mkubwa sana ktk sekta ya Afya.
Watu wengi wenye hekima wamelima mashamba makubwa ya mchaichai kwa ajili ya tiba.

Huu Mmea kuna Magonjwa unatibu ambayo hayatibiki kirahisi kwa dawa za kisasa.. ila yanakuja kutibiwa na mmea huu , ambao ni maarufu kwa matumizi ya chai

Mmea huu una virutubisho, madini na vitamn kama ifuatavyo

Energy (Nishati)
• Wanga (Carbohydrates )
• Protein (protini)
• Fat (Mafuta)
• Folates
• Niacin (Vitamn B3)
• Pyridoxine (Vitamn B6)
• Riboflavin (Vitamn B2)
• Thiamin (Vitamin B1)
• Vitamin A 6
• Vitamin C
• Madini ya Sodium 6
• Madini ya Potassium
• Madini ya Calcium
• Una madini ya Copper (shaba)
• Madini ya Iron (chuma)
• Madini ya Magnesium
• Pia madini ya Manganese
• Madini ya Selenium
Na madini ya Zinc

Hivyo huu fanya mmea huu kuwa na faida kubwa mnoo mwilini

Ukianza kuchambua kila kimojawapo hapo , utajikuta mwili umejaa kila hitaji linalohitajika

FAIDA ZA KUTUMIA MCHAICHI

🌹 Ina sifa ya Antidepressant

Matumizi ya Mafuta ya mchaichai huongeza kujistahi, kujiamini, matumaini, nguvu ya kiakili,.. Hii inaweza kusaidia sana kuondoa unyogovu kutokana na kushindwa katika kazi, maisha ya kibinafsi, wasiwasi , upweke, vilio, kifo katika familia, na sababu nyingine nyingi... Mafuta ya asili ya mchaichai ukijipaka tu hata kama ulikuwa na hofu , mshituko kama wa msiba , hali hiyo ikikutokea paka haya mafuta utakaa sawa

🌹Kupunguza Uzito

Mchaichai una citral, ambayo ni bora dhidi ya fetma.. Inapunguza mkusanyiko wa mafuta ya tumbo na kukuza utumiaji wa nishati iliyohifadhiwa, ambayo husaidia kuzuia kupata uzito unaosababishwa na ulaji mbaya wa chakula bila mpangilio ,Mtu anakula mara tano , badala ya mara moja au mbili kwa siku ,pia huongeza oxidation ya asidi ya mafuta katika mwili.

Ina sifa ya kupambana na Saratani

Citral ni kemikali iliyo ktk Mchaichai, inaweza kuwa na ufanisi katika kuzuia ukuaji wa seli za saratani bila kuathiri seli za afya za mwili. Citral n nzur katika kuzuia ukuaji wa seli za saratani ya ini na kuzuia ukuaji zaidi wa seli za saratani..

🌹Huondoa Matatizo ya Kupumua

Mchaichai hutumiwa sana katika dawa ya Ayurvedic ... Huondoa madhara ya vidonge vinavyohusika na katika kutibu kikohozi na baridi yabis . Lakin pia vitamini C iliyoko ktk mchaichai , inasaidia katika kutoa unafuu kutokana na kuziba kwa pua, mafua, na matatizo mengine ya kupumua kama vile pumu ..

Hudhibiti Kisukari
Mchaichai ni Utafiti unaonyesha ni kwa ajili ya kutibu kisukari aina ya 2. Citral iliyopo ktk mchaichai inasaidia kudumisha viwango bora vya insulini na kuboresha uvumilivu wa glukosi mwilini na kuifanya kuwa bora kwa watu wenye kisukali aina ya 2

Mambo Mengine ambayo yanatibiwa na huu Mmea

🌹Inasaidia kwenye mmeng’enyo wa chakula kama vile kuvimbiwa na gesi.
🌹Kusafisha mwili na kutoa sumu
🌹Kuboresha afya ya ngozi
🌹Kupunguza mafua na kikohozi
🌹Inapunguza maumivu na kuvimba
🌹Huongeza Kinga za mwili
🌹Huzuia Kuvu
🌹Inatatua tatizo la kugombana Kwa mke na Mme
🌹Ni nzuri kwa magonjwa ya tumbo
🌹Ukiuchanganya na Mmea wa Mziwaziwa unatibu UTI sugu iliyoshindikaña
🌹Mafuta ya mchai Chai ni mazuri kwa

Mapunye, fangasi nk. Mafuta ya mchaichai ni dawa. kuna wakati watoto wanakuja na mapunye toka shule uko, wakati mwingine minyoo tu inakuletea fangasi au ndio mambo ya kujaribisha mitumba… unatoka na ugonjwa wa ngozi hapo au utangotango….

🌹Mchaichai una kiwango kikubwa cha Catechins ambacho husaidia mishipa ya damu kuzalisha Nitric Oxide (NO), ambayo husaidia kutanua mishipa ya damu ikiwepo mishipa ya damu ktk uume.

🌹Pia mchaichai husaidia uzalishaji wa antioxidants ambazo husaidia kuondoa sumu mwilini..

🌹Mwanamke ukimchanganyia mme wako Chai ya Kijiko 1 karafuu + tangawizi + Mchaichai + Mdalasini+ Iliki

Mpe Kikombe 1 Asubuhi na Jioni baada ya wiki Mbili , Njoo Utoe Ushuhuda
 
Back
Top Bottom