Faida za tunda la ukwaju

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
FAIDA ZA JUISI YA UKWAJU
]

Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.


NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU

Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets
  • Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu
  • Baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni
  • Uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu
  • Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe
  • Andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
  • Weka sukari kwa kiasi unachopendelea
  • Pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste
  • Weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa
FAIDA YA JUISI YA UKWAJU
  • Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  • Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  • Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  • Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  • Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  • Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  • Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  • Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  • Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  • Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)
NB: Ikiwa ukwaju na asali havikudhuru, basi changanya hivyo viwili ili kupata faida maradufu!
 
MZEE HABARI NZURI LAKINI HAILEWEKI KABISA, IMECHANGANYIKA MNO, SIJUHI ULITUMIA TRANSLATOR KUITAFSIRI HII KUTOKA KATIKA LUGHA YAKE ORIGINAL (ARABIC), KAMA UMEIELEWA HII HABARI BASI UNGETUWEKEA SUMMARY YA UNACHOKIJUA

HIZI DAWA ZA ASILI NI MUHIMU SANA, MIMI NINA MKWAJU NYUMBANI KWANGU HIVYO NILITAKA KUJUA uZURI FAIDA ZAKE
 

mkuu,
nije unigawie kidogo?
 
Faida nyingine ya Ukwaju: Juisi ya Ukwaju inasaidia wale wenye mgandamano wa Choo, yaani kutokwenda haja kubwa muda mrefu. Ukiinywa ni lazima ukaripoti Ofisi Kuu Toilet
 
sasa nimeelewa maana kule kwetu "ukwaju" ni kitu kingine pia. Labda faida nyingine ni mazoezi ya kukunja sura wakati wa kula /kunywa.

kitu gani na kikoje?
Sasa c tutanekana wazee sura zikikunjamana jamani!
 
[FONT=Arial,Helvetica,Geneva,Swiss,SunSans-Regular]Attributed Medicinal Properties[/FONT][FONT=Times New Roman,Georgia,Times]Tamarind is considered a mild laxative and digestive. It is used to treat bronchial disorders and gargling with tamarind water is recommended for a sore throat. It is antiseptic, used in eye-baths and for the treatment of ulcers. Being highly acidic, it is a refrigerant (cooling in the heat) and febrifuge (for fighting fevers). The Ananga Ranga suggests consuming tamarind for enhancing a woman's sexual enjoyment.

[/FONT]
 
Wife huwa anautumia kuondoa mambo ya kutapika
Very useful infact dawa za kienyeji ni very useful.
Kuna jamaa yangu kpona ulcers ivi ivi
 
Samahanini Wakuu nimejaribu kutafisiri kutoka Lugha ya kiarabu kwenda kiswahili ni hivi kwa ufupi Ukwaju una faida nyingi sana kwa Binadamu Husaidia kutibu maradhi ya shinikizo la damu,
kutapika, kichefuchefu na maumivu ya

kichwa.na hili neno
Tamarind ni lugha ya

kiingereza kwa Kiswahili ni Ukwaju.
 
embu jaribu kuiweka kwenye google translator na kuirejeza lugha ya awali labda utaelewa kamanda, si unajua tena copy n paste saa zingine...:smile-big:
BTW kazi ni nzuri na ni faida imeonekana bila kujali upotofu wa lugha.
 
Sasa nimeelewa maana kule kwetu "ukwaju" ni kitu kingine pia. Labda faida nyingine ni mazoezi ya kukunja sura wakati wa kula /kunywa.

:smile-big::smile-big::smile-big:
 
very interesting and useful though imenichukua muda kuunganisha maneno,ukwaju is very helpful indeed mi nilikua najua tu kule kwa bibi zangu wanatumia,infact tz tumejaaliwa vitu vingi vya asili na safe sema hatuna elimu ya kuelezea hivi mnajua hata majani ya mpera ukitafuna ni dawa nzuri sana kwa tumbo.
 

OOOOH MSICHANA SUKARI....ULISHAJITAMBULISHA LAKINI WEWE?:A S-heart-2:
 
naomba msaada wa kufaham kama matunda ya ukwaju yanaweza kutumika kama dawa na ni dawa ya kutibu nin?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…