Faida zipatikanazo kutokana na kunywa maziwa

Faida zipatikanazo kutokana na kunywa maziwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MARA nyingi watu wengi wamezoea kula au kunywa kile kinachopatikana na si kile kinachotakikana (kinachohitajiwa). Tabia hii huchangiwa na mambo mengi kama ukosefu wa fedha, muda wa maandalizi, mila na desturi

pamoja na sababu hizo, moja kubwa linalochangia ni ukosefu wa elimu sahihi ya vyakula. Bila ya kujua faida ya kitu unachofanya au unachotaka kufanya hakika hautatilia mkazo. Baada ya kuona aina za maziwa huko nyuma, leo tuyaangalie faida zake katika miili yetu.

MAZIWA kama yalivyo hayawezi kutengenezwa kiwandani. Ni lazima yatokane na wanyama hasa wanyama wanyonyeshao (Mamals). Na hayapatikani pasina wanyama kuzaa, hivyo kuhitajika kumnyonyesha mwana. Na sehemu katika lishe ya mwanae

ndio sisi huitumia. Na kwa minajili hiyo, basi maziwa ni lishe tosha. Ndugu msomaji hata kabla ya kueleza faida tuzipatazo kutokana na maziwa, hebu tumfikirie mtoto mchanga. Mtoto aliyezaliwa leo anaishi kwa kunyonya tu takriban miezi minne au sita. Bila

mjadala ni kwamba maziwa yamebeba mahitajio yote muhimu katika kujenga mwili, kuupa mwili nguvu na joto na kuulinda mwili na magonjwa.

Maziwa hutupatia takriban vitamini zote ambazo huyeyuka kwenye mafuta. Nazo ni vitamini A, D, E na K. Vitamini A huhusika na shughuli mbalimbali mwilini. Mfano afya bora ya ngozi zetu kuwa nyororo na ng'avu na pia kuwa na uwezo wa kuzuia wadudu

wasiingie mwilini. Vile vile vitamini A hutumika pia kuyapatia macho uimara wa kuona. Na hasa kuona usiku au kwenye mwanga hafifu. Ukosefu wake hudhoofisha macho na hata kuleta upofu, ngozi kusinyaa na kuonekana iliyozeeka hata kama ni ya kijana.

Vitamini D husaidia mwili kuweza kufyonza madini ya kalsiamu. Bila kuwepo vitamni D kalsium hupotea bure kwa kutolewa nje kama kitu kichohitajika. Japokuwa vitamini D tunaweza kuipata kwenye jua la asubuhi, watu wengi hawawezi kulipata jua hilo.

Labda kwa kuishi magorofani au chini ya milima au kutoweza kutoka nje nyakati za asubuhi. Hivyo ni bora kujiwekea uhakika wa kupata vitamini D kwa kunywa maziwa.

Umuhimu wa madini ya Calcium ni kiungo muhimu katika ujengaji wa mifupa. Hasa kwa wajawazito na watoto ambao mifupa yao bado inajengeka. Mwili imara hubebwa na mifupa imara. Na mifupa imara inajengwa na madini ya Kalsium. Ni bora kujijengea

mifupa imara, meno na sehemu ya mifupa. Hakika kila mtu anahitaji meno bora na imara, vile vile kalsium hutumika katika misuli (muscle) wakati wa kujikunja na kunyooka. Pia husaidia katika mtandao wa ufahamu mwilini (nerve conduction). Kwa ufupi hayo ni manufaa ya kunywa maziwa, samaki na kadhalika. Mbali na Kalsium maziwa hutupatia madini ya salfa, sodium na phosphoras ambayo mwili pia huhitaji kwa kazi zake mbalimbali.

Maziwa pia hutupatia protini kwa ujengaji wa miili yetu. Mathalan mtoto mdogo wa siku moja huongeza ukubwa na uzito kwa kunywa au kunyonya maziwa tu. Japokuwa kiwango cha protini hutofautiana kulingana na mnyama, pia maziwa ya ng'ombe yana protini ya kutosha. Hali kadhalika katika maziwa ya mbuzi na kadhalika.

Maziwa pia hutupatia sukari (wanga) japo kwa kiasi kidogo lakini kidogo chafaa kuliko kukosa. Na ndio maana japo kwa kunywa maziwa waweza kuhisi nguvu iwapo ulikuwa na njaa.

Nyakati za baridi, maziwa hutumika kama kinywaji moto. Yenyewe peke yake kwenye chai, kahawa au tangawizi. Na wakati wa joto, maziwa hutumika kama kipozeo na kiburudisho tosha. Na kwa nyakati hizi, kila sehemu inaweza kupatikana na maziwa. Kwa asiyependa tunamshauri aanze kuyapenda na kuyatumia.

Maziwa pia hutumika kama dawa kwa kuchanganywa na vitu mbalimbali. Mathalani maziwa ya mama yakamuliwapo kwenye jicho linalowasha, uchafu hotoka na kujihisi salama.

Kwa kuzingatia umuhimu wa maziwa kama tulivyoona kwa ufupi, kwa kauli moja tunaisisitiza jamii kunywa maziwa katika milo ya kila siku. Na vile vile kama kiburudisho wakati wowote. Ni hasara kupoteza fedha zako kununua vinywaji visivyo na faida kubwa

kama tuipatavyo katika maziwa, mathalan soda, na juice za makopo ambazo zimejaa rangi, maji na sukari na madawa bila ya virutubisho vyovyote vingine. Tumia pesa zako kwa malengo maalum. Jenga afya yako, kunywa maziwa.


NINATAMANI MAREHEMU MAMA YANGU MZAZI AWE HAI NINYONYE MAZIWA YAKE KUMBE MAZIWA YA MAMA YANA FAIDA NAMNA HII AHHH JAMANI WATOTO WANAFAIDI KWELI.



Mkuu Boflo alivyokuwa mtoto anavyomsumbuwa mama wake. Ee jamani tuwaheshimuni wazazi wetu jamani.
 
Last edited by a moderator:
Wewe kama mama, umemzaa mtoto....
unategemea nini???
Ni lazima umpe mahitaji yake ya msingi
kama chakula, malezi, elimu nk
Na kwa nn unazaa kama huna uwezo????
Na kwa nini utake mtoto akiwa mkubwa
lazima alipe fadhila!!
 
Boflo wewe ni yupi hapa?
avatar21062_29.gif
 
Last edited by a moderator:
kabanga mimi akili ilinihama nilipoona avatar ya Boflo hadi nikasahau kuchangia,
eti MziziMkavu mbona nasikia maziwa ya ng'ombe yana ugonjwa kama hayajatiritiwa vizuri je hi ni kweli?
na kwa ng'ombe wa sasa ambao wanaishi kwa dawa itakuwaje hayo maziwa yake?

lakini maziwa haya natumaini yasiwe yale yamewekwa maji mengi...Eti jamani?
 
Last edited by a moderator:
[h=1]Unywaji maziwa bado tatizo Tanzania:[/h]
KWA UFUPI
  • Akaongeza kuwa viwango vinavyopendekezwa kimataifa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na lile la Chakula na Kilimo (FAO) ni lita 200 kwa mtu kwa mwaka ambazo zinakaribiwa na Kenya wanaokunywa lita 140.
Songea. Kila mwezi Mei Watanzania huungana na wenzao katika kuadhimisha Wiki ya Unywaji Maziwa.

Katika maadhimisho hayo, imebainika kuwa Watanzania bado wako nyuma katika unywaji wa maziwa ikilinganishwa na Kenya au nchi nyingine zilizoendelea kama Uholanzi na New Zealand.

Mwambungu, kwa upande wake akawataka wananchi kujenga utamaduni wa kupenda kunywa maziwa kila siku badala ya kusubiri wang'atwe na nyoka au wadudu ama washauriwe na madaktari.

Akasema Mwambungu kuwa watu wengi wamekuwa wavivu katika suala la unywaji wa maziwa ikilinganishwa na kasi wanayoitumia kwenye unywaji wa pombe ambapo baadhi yao wamekuwa mabingwa wa kushinda au kukesha baa.

"Kama ningekuwa daktari, ningetamani kumweleza kila mgonjwa anayekuja hospitali kupata matibabu kwamba ili apone vizuri anatakiwa kwanza kunywa maziwa. Ninadhani wengi wangefanya hivyo," akasema Mwambungu. Akaongeza kuwa kasi ya unywaji wa maziwa mkoani Ruvuma ni wastani na lita 11.6 kwa mtu kwa mwaka na kuongeza kwamba takwimu za uzalishaji wa maziwa na unywaji wake nchini zinaonyesha kuwa Watanzania hutumia wastani wa lita 45 kwa mwaka.

Akaongeza kuwa viwango vinavyopendekezwa kimataifa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na lile la Chakula na Kilimo (FAO) ni lita 200 kwa mtu kwa mwaka ambazo zinakaribiwa na Kenya wanaokunywa lita 140.

Kutokana na hali hiyo, RC Mwambgungu akawataka wananchi wa mkoa wake kuyatumia maadhimisho hayo kama darasa katika kujifunza mbinu bora za ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na usindikaji wa maziwa kwa ajili ya kuinua kiwango cha upatikanaji wa maziwa hayo.

Pia, aliwaasa wananchi hao kuacha kasumba kuwa kunywa maziwa ni mpaka mtu augue.

Akasema kuwa serikali itaendelea kuboresha sekta ya maziwa ili iendelee kutoa matokeo chanya na hatimaye kuhamasisha wananchi wengi kufuga ngombe wa maziwa kwa lengo la kuboresha afya kwa kunywa maziwa na kuongeza kipato na uchumi wa kaya na hatimaye taifa. Aliishauri Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi haina budi kuanzisha mradi wa maziwa katika shule nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Maziwa, Hamis Mzee alisema kuwa maadhimisho hayo yalipelekwa Ruvuma baada ya kufanya tathmini na kuona mwamko wa unywaji maziwa ni mdogo.

Aliwataka wananchi hao kujenga utamaduni wa kuchemsha maziwa kabla ya kuyanywa ambapo alieleza kwamba familia isiyopenda kunywa maziwa ukuaji wake unakuwa wa shida.

Aidha, wananchi Ruvuma wakaitaka Kampuni ya Asas Dairies kupeleka huduma zake mkoani humo ili waweze kunufaika na huduma hiyo.


Katika maonyesho ya yaliyo fanyika Mkoani Ruvuma Mei 29 hadi Juni Mosi 2013 kwenye viwanja vya Manispaa Songea, baadhi ya wazalishaji na wasindikaji wa maziwa ikiwamo Kampuni ya Asas ya mjini Iringa walishiriki.

Asas, kwa upande wao ilijinyakulia medali tano (5), mbili za dhahabu , moja ya fedha , moja ya ushiriki na moja ya ushindi wa jumla.

Ushindi huo wa kishindo ulitarajiwa na wengi ambao walijaa katika banda la Asas kwa lengo la kununua na kuuliza mambo mbalimbali kuhusu bidhaa za kampuni hiyo.

Mafanikio yao

Asas Dairies kwa upande wake ikaeleza kuwa inajivunia ubora wa bidhaa zake ambazo zinapendwa na kutumiwa.

Unywaji maziwa bado tatizo Tanzania - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz
 
Mkuu nimekua na tatizo , ninapotumia maziwa zikifika kuanzia siku tatu mfululizo naanza kuhisi maumivu sehemu ya haja kubwa
 
Hello Jf

Nimekuwa Mtumiaji Wa Maziwa Fresh Kwa Muda Mrefu, Ila Bado Napenda Kujua Faida Zaidi Za Maziwa Yenyewe. Je, Sehemu Ya Mlo Kamili?
 
Hello Jf

Nimekuwa Mtumiaji Wa Maziwa Fresh Kwa Muda Mrefu, Ila Bado Napenda Kujua Faida Zaidi Za Maziwa Yenyewe. Je, Sehemu Ya Mlo Kamili?
Inaongeza nguvu kwenye mifupa, kukufanya kunya vizuri yaani unakunya kwa raha zako mwenyewe bila kinyesi chako kuwa kigumu, kukupa hamu ya kula na kwa wanaume wa Dar, kuongeza hamu ya tendo la ndoa bila kujipiga vidole mwenyewe.
 
Kutokana na mafundisho ya Mwl wako je maziwa hayana gesi?
 
Back
Top Bottom