Fainali ya ASFC, uwanja utakao tumika ni aibu

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Wakuu Habarini.

Nimeona Na Kushangazwa na Uwanja Wa Lake Tanganyika Kigoma Ambao utatumia katika Fainali za ASFC, Huu sio Uwanja wa Mpira na Pori na Mapagale Ya Uwanja.

Sifikiri wala sioni huu uwanja ukikamilika Hivi Karibu, Kuna Uwezakano mkubwa sana Wa Fainali hizi Kuihusisha SIMBA NA YANGA lakini Kwa Kiwanja hicho Tutashuhudia Fainali Mbovu kuwahi kutokea Nchi Kwetu.

Ikiwa Muda mchache umebaki kuifikia Fainali na Uwanja Umeanza Kulimwa sasa, Najiuliza huu uwanja utakamilika lini na Kufanyiwa Majaribio Lini kwa Ubovu wa Pitch Ile, Hakuna Vyumba Vya kubadirishia nguo na hata njia za kukimbilia ndio zinalimwa sasa.

Kama walijua Ule uwanja utatutumika kwa Fainali za ASFC walikuwa Wapi kurekebisha Kwa Mwaka Mzima. Kwa Ule Uwanja Hauhitaji marekebisho ya Miezi miwili au 3 unahitaji miaka hata 2.

Anaye washauri TFF ni nani?
 
Uwanja Nelson Mandela,Sumbawanga ulirekebishwa na ukatumika kwa fainali kama hizi.,Lakini pia ikumbukwe mwenyeji Serikali na wadau wa soka katika mji wa Sumbawanga walikuwa na utashi,na walikaribisha timu yeyote ije Sumbawanga na kuutumia uwanja wao wa nyumbani.

Kama Kigoma,Serikali na wadau hawana mwamko wa kuvutia wapenzi na wadau wa soka kushiriki na kusaidia kuharakisha ukarabati wa uwanja,basi hilo litakuwa ni uzembe na bahati mbaya kwa wapenzi wa soka waliopo Kigoma na maeneo jirani.

Lakini,nakumbuka mdhamini wa mashindano amekuwa mstari wa mbele katika kuandaa viwanja vya fainali za mashindano.

Sina shaka muda ukifika, uwanja utakuwa tayari kwa fainali.
 
TFF na Bodi ya ligi hawako serious, huwa wanakurupuka tu kujiamulia mambo yao, hakuna sababu kupeleka fainali mikoa tofauti hata kama mikoa hiyo haina viwanja vizuri.

TFF wawe wakweli kuwaambia tulitaka kupeleka mkoa fulani lakini uwanja wao mbovu hivyo tumehamishia mkoa mwingine, hili litasaidia hao jamaa kukarabati viwanja vyao hasa sehemu ya kuchezea.
 
Mpaka sasa uwanja wa Nelson Mandela haufai kuchezea fainali.Hiyo rekebisha iliyofanyika bado haujawa uwanja bora hata kwa ligi haufai ni basi tu.

TFF wanazingua tu, hakuna uwanja nje ya dar isipokuwa kaitaba unaofaa kuchezea fainali. TFF ni kama hawapo kwa ajili ya soka maana huwezi kupeleka fainali kwenye uwanja usio bora wakati una viwanja bora kwa sababu yoyote ile.

Ile sababu ya kusema sijui tunapeleka mwamko mkoa husika ni sababu mfu maana kuna uwezekano wa kupunguza mwamko kwa mashabiki watakao ona kwenye tv mechi ikichezwa kwenye uwanja usio bora.
 
Tiefuefu hawako serious na hela zetu
 
TFF na Bodi ya ligi hawako serious, huwa wanakurupuka tu kujiamulia mambo yao, hakuna sababu kupeleka fainali mikoa tofauti hata kama mikoa hiyo haina viwanja vizuri...
hiii janja fainal kuja dar kwa kisingizio hicho
 
Wekeni picha tuone ilo shokola...ili tuwatukane vizuri hawa tifuatufua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…