Fainali ya ASFC | Yanga SC 3 (4) - 3 (1) Coastal Union | Uwanja wa Sheikh Amri Abeid | Yanga BINGWA

Duh karne hii bado unaamini uchawi katika soccer acha ujinga wewe.
Uchawi umetajwa Hadi kwenye biblia kama hutaki watu waamini uchawi Basi wasiamini pia biblia maana ni karne nyingine pia hii

Costal wamevunja nazi sana.
 
81' Makambo Goooooooooooooaaal gooal

Makambo anaipatia Yanga SC bao la pili, shuti kali la kimo cha mbuzi linamuacha golikipa Mussa akichumpa bila mafanikio

Yanga SC 2-1 Coastal Union
 
Tafadhalini viongozi wa Yanga, huyu Heritiel Makambo mwacheni amalizie tu amalizie makataba wake.

What a sub! Yaani katoa assist, na pia ameitanguliza timu yake mbele baada ya kuwa nyuma kwa goli 1-0!!



Dah! Hiki Kisopu kama kichawi vile!! ☹️
 
88' Sopu Goooooooooooaaal goal

Abdul Sopu anaipatia Coastal Union bao la pili, akijitwisha kichwa na kumuacha golikipa Diara akiangalia tu, Kijana hatari sana.

Yanga SC 2-2 Coastal Union
 
Japo ningetamani Yanga afungwe leo ila kiukweli Hawa wagosi hawawezi kumfunga Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…