Fainali ya CRDB shirikisho kupelekwa Zanzibar ni dharau kwa mashabiki wa Simba

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
18,360
Reaction score
26,244
Ni jambo la ajabu, Zanzibar waba ligi yao, chama chao cha soka, mamlaka yao ya mapato lakini ama kw kujipendekeza kwa wanasiasa au mpango wa mwenyekiti wa bodi ya ligi kulinda maslahi ya Azam.
Mashabiki wa Simba wengi wao wakiwa upande wa bara wamekuwa wakijitoa muda mrefu ikiwemo kuchangia faini za Simba wanazopigw CAF lakini viongozi wao wamekaa kimya badala ya kuwatetea.
 
Inabidi huu upumbavu uzuiwe ..Mbona sijawahi ona hao watu wa huko visiwqni wakileta mechi zao huku bara.

Naona huu upumbavu unaendekezwa sasa kwa bidii.Team sio za Zanzibar ila ndo kila wakati mechi zinapelekwa huko.

Wale wana mashindano yao na ligi zao.

TFF achani huu upumbavu ..Tunajipendekeza sana kwa Wazanzibara
 
Hii mipira ya Tanzania imejaa siasa tu ndo maana mm nimeacha hata kwenda uwanjani
 
Aly kamwe anahusikaje na upangaji wa ratiba, hoja kwanini timu za bara zinashiriki mashindano ya bara fainali ziende kuchezwa visiwani.
Shida ukiona jina la Ali Kamwe unapagawa. nimekupa kanuni ya 9(6) husomi umekimbilia koja ndogo isiyokuwa na maana yoyote
 
Shida ukiona jina la Ali Kamwe unapagawa. nimekupa kanuni ya 9(6) husomi umekimbilia koja ndogo isiyokuwa na maana yoyote
Ndio maana hizi timu zinatumiwa kudumaza akili, wazanzibar wanawatawala watanganyika kupitia akili kama zako.
Hapa tunazungumzia bamba kila kitu cha Tanganyika kinavyotumika kumnufaisha mzanzibar.
Kana mechi ingechezwa Tanganyika mapato yangeenda Tra
Watu wangefanya biashara ya malazi, chakula na vinywaji lakini wewe umejikita kwenye hoja ya usimba na uyanga.
 
Sio dharau kwa simba hii ni dharau dhidi ya Watanzania bara!!, Zanzibar inajitegemea kwa ligi yake na mambo ya mpira, hizo tartibu na kanuni zinatoka wapi watu kupelekwa maeneo ambayo sio asilia na mpira wetu?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…