Fainali ya UEFA inapoteza mvuto

Fainali ya UEFA inapoteza mvuto

DR SANTOS

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
12,846
Reaction score
28,106
Tofauti na fainali zingine zilizopita, hii imetokea kuwa ni yenye ushindani sana ukizingatia timu zenye mastar wa dunia namaanisha juventus wakiwa na cr7
Na fc Barcelona wakiwa na lionel messi

Zimetolewa. Wengi tulitarajia, fainali ingechezwa kati ya Barcelona na ajax lakini timu zote zimetokea kupindua matokeo na kuishangaza dunia.

Si mara ya kwanza kwa Liverpool kupindua matokeo katika michuano mikubwa
Liverpool vs Dortmund
ambapo Liverpool aliweza kushinda goli NNE pale an field

Na mwaka 2005 dhidi ya Ac milan.
Na matokeo yote yameonekana kupinduliwa katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool
Anfield.

Uwanja wa anfiled inaaminika Luna nguvu ya miujiza ambayo inatokana na kocha alieiongoza Liverpool kwa mafanikio makubwa kabisa, sir bill shanky, ambaye baada ya kufariki dunia mwaka 1981
Mwili wake uliteketezwa na majivu take kuzungushwa katika chaki za uwanja.

Pengine hii ndiyo sababu kubwa liverpool inakua na morali hasa katika mechi zake za nyumbani
[emoji818][emoji818][emoji818][emoji818]

Upande wa Tottenham hotspurs in timu ambayo msimu huu haijasajili na wachezaji wake sio wa gharama kubwa ukilinganisha na timu za pale england kama Manchester united man city na Chelsea
Lakini kwa miaka mitatu mfululizo wamekua wapinzani wakubwa kwenye ligi ya uingereza na kupelekea timu kama arsenal kukosa kushiriki mashindano ya uefa
Kwa miaka mitatu mfululizo.
Wachezaji wa spurs wanacheza kwa kujituma sana.

Tutarajie mengi sana katika fainali ya uefa japo ni TIMU ZA england ndo zinacheza.

Allez allez allez.
#UCL
 
Mtoa mada utakuwa umeanza kuangalia kabumbu 2010, hivi kuna fainali mbovu kuwahi kutokea kama ile ya mwaka 2004, Porto Vs As Monaco

Porto ya akina Calvalho, Paulo Ferreira, Thiago Mendes walikuwa wanapaki basi chini ya jemedari Mourinho kisha unakutana na As Monaco ya akina Evra, Ludovic Giuly ambayo atleast walikuwa wanacheza soka japo sio zuri.

Fainali hii ya mwaka huu itakuwa nzuri tu Spurs inacheza soka la kuvutia safi hivyo hivyo kwa Liverpool. Labda kinachokusumbua ni hizo timu zako pendwa kutokufika fainali.
 
Binadamu tunakuwa wagumu sana kukubaliana na swala la mabadiliko.

Wakati wa Barca na Madrid kuitawala UEFA umekwisha, kilichoumaliza wakati huo ni kuisha kwa Messi na Ronaldo.

Tukubaliane na swala la kwamba sasa ni wakati wa timu za Uingereza, na hili limetokana na mkataba mkubwa sana wa Broadcasting ambapo unazipa timu hela nyingi, pia uwekezaji wa matajiri wakubwa kwenye timu hizi kiasi cha kuweza kuchukua makocha bora duniani na wachezaji pia.

Ukizungumza Top 5 best coaches kwa sasa, Pep, Klopp na Pocchetino hawatakosa, Mourinho yuko bench lakini naye alikuwa hapo hapo, Emery pia ni elite coach naye yuko hapo. Hivyo ligi imeongeza sana ushindani na ubora kwa kipindi cha karibuni.

Leo hii UEFA na Europa zinacheza All English Teams, ni massive development kwa EPL.

NB: Kwa miaka 13 iliyopita, Messi na Ronaldo wamelichukua kombe mara 9 (2006, 2008, 2009, 2011, 2014, 2015, 2016, 2017 na 2018). Kupoteza kwao ushawishi kwa sababu ya umri lazima kuathiri vilabu wanavyovitumikia.
 
Fainali za UEFA Champion League hazijapoteza mvuto, fainali za mwaka huu zimekuwa na msisimko mkubwa toka hatua ya mtoano mpaka kufikia sasa. Kutolewa kwa Real Madrid na Juventus Turin na timu ile ile Ajax Amsterdam ni msisimko mkubwa kwenye mchezo wa soka.
Lakini Kitendo cha EPL kuingiza timu zake zote 4 kwenye hatua ya robo fainali na hatimaye timu mbili za ligi hiyo kukutana kwenye fainali ni dhahiri sasa ligi hiyo iko vizuri.
Vinginevyo timu zinazotegemea huduma ya Messi na CR7 zimeacha kucheza mpira wa kitimu na kuwabebesha majukumu yote nyota hao.
Ilikuwa rahisi sana kwa Ajax kuiangusha Juve na Liverpool kuiondoa Barcelona maana timu hizo zimeacha kucheza mpira wa pamoja na kutegemea vipaji vya mastaa wake hao.
 
Back
Top Bottom