Fainali za Ndumbaro CUP Bingwa Aondoka na Ng'ombe

Fainali za Ndumbaro CUP Bingwa Aondoka na Ng'ombe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Desemba 25, 2024 Songea Mjini ameshuhudia fainali za Kombe la Ndumbaro CUP katika uwanja wa Chuo cha Matabibu Songea (RMA)

Fainali za Kombe la Ndumbaro CUP imefanyika kati ya timu ya Bombambili na Liwena ambapo Bombambili wameibuka bingwa wa mashindano hayo huku wakijinyakulia zawadi ya Ng’ombe na Seti ya Jezi

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Mhe. Ndumbaro amewapongeza Bombambili kwa kuibuka mabingwa huku akitangaza ratiba ya mashindano hayo kwa mwaka 2025 kuanzia mwezi Aprili na zawadi ambapo mshindi wa kwanza atapata kitita cha Shilingi Milioni Tatu, Mshundi wa pili milioni mbili na mshindi wa tatu milioni Moja.
 
Back
Top Bottom