Faisal asinyimwe kuvaa medali ya ubingwa

Faisal asinyimwe kuvaa medali ya ubingwa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ubingwa huu wa Yanga una mchango mkubwa wa mtukutu Fei Toto. Jasho lake ni jingi mno kwenye msimamo wa ligi.

Aitwe ashiriki kuvaa medali sawa na wenzake.
 
Ubingwa huu wa Yanga una mchango mkubwa wa mtukutu Fei Toto. Jasho lake ni jingi mno kwenye msimamo wa ligi.

Aitwe ashiriki kuvaa medali sawa na wenzake.
Nani alimfukuza? Mtoto mtoro. Hata hivyo hata akivaa hawezi kuwa na raha kama wenzake, yaani anavalia nyumbani huku Dom limevimba Kama kaumwa na nyigu.
 
Hata akiitwa atakubali??
Medali yake apekekewe hata nyumbani kwao. Anachokifanya Fei sio akili yake hata kidogo, maana kunguru Hana kibiyongo. Kuna watu na taasisi kubwa kabisa zimemdhulumu huyu mtoto kumnyima furaha na fursa huyu mtoto wakidhani pesa inaweza kununua kila kitu. Inawezekana hawa watu wanamlipa Fei hata bila kucheza huko nyumbani aliko na kusahau kuwa pesa sio kila kitu kwa kijana. Furaha kubwa ya kila mchezaji ni kuvaa medali na kunyanyua makwapa. Kuna wachezaji wanachama timu kwasababu ya kukosa kuvaa medali na kunyanyua makwapa.
 
Kwani tangu ameondoka kuna kilichoharibika?
Magoli yake hayatafutwa na TFF Wala CAF. Points za magoli yake huenda ndio yaliyosababisha Yanga tutangaze ubingwa kabla ya mechi 2.

Hii itaonyesha kuwa Yanga ni next level, wamwite TU avae medal ila kutofautisha Yanga na timu nyingine.
 
Ubingwa huu wa Yanga una mchango mkubwa wa mtukutu Fei Toto. Jasho lake ni jingi mno kwenye msimamo wa ligi.

Aitwe ashiriki kuvaa medali sawa na wenzake.
Ataivaa hiyo medali akiwa huko kwao Mchamba wima, au akiwa uwanjani na wachezaji wa Yanga walioipigania timu yao mwanzo mwisho?

Yusuph Bakhresa amuite siku ya fainali ya ASFC ili ampe medali yake ya mshindi wa pili.
 
Anzisha timu yako uipe ubingwa afu umpeleke hiyo medali....!!, Dawa ya jeuri ni jeuri.
 
Yanga ni zaidi ya Fei Toto hata wanaomrubuni wamejifunza hilo, Nina uhakika kuwa hata wao Sasa hivi they feel guilty kwa kitendo walichomfanyia mtoto mdogo ambae bado anajitafuta.
 
Magoli yake hayatafutwa na TFF Wala CAF. Points za magoli yake huenda ndio yaliyosababisha Yanga tutangaze ubingwa kabla ya mechi 2.

Hii itaonyesha kuwa Yanga ni next level, wamwite TU avae medal ila kutofautisha Yanga na timu nyingine.
Unadhani kwanini wamuite? Kwani walimfukuza? LAbda kama kila mchezaji ataitwa..!!
 
Back
Top Bottom