Faiza Ally (Ex wa Mheshimiwa), awajibu Wambea

Faiza Ally (Ex wa Mheshimiwa), awajibu Wambea

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
SUGUNAMWANAYE.jpg

Picha aliyoweka Faiza Ally Instagram ya Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu'
akiwa katika pozi na mwanaye Sasha.



MSANII wa filamu Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu', leo amewatolea uvuvi watu waliokuwa wakijiuliza maswali kuhusu mwanaye Sasha na na baba yake.

faiza.JPG


Baada ya kuweka picha ya Sugu na mwanaye, Faiza Ally aliandika haya.


Kupita akaunti yake ya Instagram, Faiza ameweka picha na Mhe. Sugu akiwa na mwanaye Sasha na kuandika kuwa "Mara nyingi huwa nawapiga picha mimi mwenyewe sema tu sipendi sana kurusha kwangu"

Na kwa wale waliokuwa wanauliza maswali juu yao, Faiza amewajibu hivi: "Ni kweli kuna wakati tulikuwa hatuelewani kabisa na wala hatukuwa tunaonana lakini kwa sasa tofauti zetu zimeisha hatuna ugomvi japo hatuko pamoja"

faiza.jpg

Faiza akiwa na Mhe. Sugu enzi hizo.


"Lakini mwisho wa siku huyo ndiyo baba Sasha na mzazi siku zote atakuwa mzazi tu, haijalishi tuna tofauti kiasi gani" Alimalizia kuandika msanii huyo asiyeishiwa vituko.

Baada ya kuweka picha hiyo wengi wa mashabiki wa Faiza walimpongeza kwa hatua hiyo huku wengine wakiwataka warudiane ili walee mtoto pamoja.
 
Kaishiwa na yeye kwani asojua ninani kama mkiwa mmezaa hata mkiachana mnabaki kua wazazi wa mtoto,
aondoe hashuo zake .............
 
Nimeipenda caption yake, leo kaongea kiutu uzima kidogo.
 
si ndio huyu alivaaga pampas sijui daipa mwenye birthday party yake?
 
Mmmmhhhh hapa nimekosea njia. Huyo Faiza ndo kwaaaanza namuona hapa. Amecheza filamu gani?
 
Mi napendaga haya maumbo wanajua sanaaa kuzungushaa sugu aliachaa karataa! Halafuu hua hawachokiii unapelekeaa fire mpakaa basiii jamaanii ugonjwaa wangu huu
 
Dada,hongera kutujuza.wazazi shirikianeni KumLea mwanenu vena.tofauti zenu kisiwe kigezo cha kuzorotesha malezi ya mtoto.
 
Back
Top Bottom