MLIMAWANYOKA
JF-Expert Member
- Oct 25, 2019
- 631
- 2,247
π
πππππ
π: ππππ ππππππππ, ππππ ππππ....!!!
π΅π. π±πππ-π©ππππππ π΄. π΅πππππππ
_______________________
Ili unielewe nitakachoongea hapa, unatakiwa uwe Mtulivu wa akili badala ya kutegemea tu D mbili. Maana unaweza ukawa na D 2 zako halafu nikaishia tu kukuchanganya.
Iko hivi, 1% tu ya Watu wote ndio Wanaongoza Dunia; 4% Vibaraka; 90% Wamelala; 5% Wanaujua ukweli na wanawaamsha 90% waliolala. Lakin 1% wanawatumia 4% kuwazuia 5% wasiwaamshe 90%
Umenielewa? Inawezekana haujanielewa kwasababu pengine na wewe ni miongoni mwa 90% ya waliolala. Twende taratibu maana nataka nikuamshe usiendelee kulala. Naomba usikate tamaa, tueleweshane.
1% πΎππππππππππ π«ππππ
Ni Asilimia moja (1%) tu ya Watu wote Duniani ndio wanaoiongoza hii Dunia. Ukweli huu unamaana kwamba, Asilimia Tisini na Tisa (99%) ya watu wote Duniani wanaongozwa na kundi ndogo sana la watu ambao ni Asilimia moja (1%) tu. Hawa ni Viongozi na Watawala.
Wanaweza kuwa ni Viongozi wa Kisiasa, Kiserikali, Kidini, Kijamii na Kiraia na katika nyanjazingine zote za Maisha ya kibinadamu. Kifupi ni kwamba, hawa ndio Viongozi wetu wanaotuongoza kwenye Jamii zetu.
Lakini pia yanaweza kuwa Makundi ya watu au Nchi zilizoendelea Kiuchumia, Kisiasa na Kijamii. Wanaweza kuwa Wafanyabiashara au Matajiri au watu walioushikiria, kuuongoza na kuuendesha Uchumia wa Dunia.
4% π½πππππππ
Hawa wanaweza wale tunaowaita Mtaani kwetu kama 'π΄ππππππ' wa Viongozi au Watawala. Au kwa Kipare cha kule kwetu Ugweno tunawaita 'π·ππππππ'. Ndio wale ambao wanayaendesha maisha yao kwa kutegemea kujipendekeza kwa Viongozi, kutegemea fadhila za Viongozi au Watawala. Ndio Watumishi wa viongozi wanaotumiwa kwa Maslahi ya Kiuongozi ya viongozi au Maslahi binafsi ya viongozi.
Hapa wapo hao Machawa, baadhi ya Watumishi wa Jeshi la polisi au baadhi ya watumishiwa Vyombo vingine vya Dola, Watumishi wa Umma, Vijana wanaotegemea Fadhila za Uteuzi, ajira, wapiga Mapambio, wafuasi, mashabiki, wafuata upepo wa Viongozi, wanazi, 'waliokunywa maji ya bendera', makada, wafia dini, na wengine wanaofanana nao.
90% πΎπππππππ
Hawa ndio watu ambao wamelala, wamezubaa, hawajui kinachoendelea. Ni wajinga wasiojua kinachoendelea. Wapo kwenye Giza la Ujinga na Dimbwi la kukosa Maarifa. Wanafichwa ukweli wa mambo yanavyoendeshwa na Viongozi. Na hawajishughulishi kuamka usingizini mwao.
Hawa ndio ambao Viongozi wanautumia Usingizi (Ujinga) wao kufanya Mambo yao ya hovyo kwasababu sio tu kwamba wapo Usingizini lakini pia hata wao wenyewe hawajui kama wapo usingizi. Ni Wajinga wasiojua kama wao ni Wajinga; wala hawajui wafanye nini kuondokana na ujinga wao.
Ni mbwa wasiokuwa na meno. Wapo usingizini wamelala usingizi; na usingizi wao hauna hata Ndoto. Ni wajinga ambao hawaijui thamani ya umoja wao, hawaijui nguvu yao kama umma. Hawajui kama wao ni wengi sana kuliko kundi lingine lolote lile. Hawaijui thamani za nguvu ya kura zao wanazozipiga kuwachagua viongozi na kuwaweka Madarakani.
Hawa sio Wafu kwamba hawaamki hata kama wakiamshwa maana hawajafa. Namaanisha sio Wapumbavu kwamba hata wakielimishwa hawaelimiko. Ni wajinga tu walioko usingizini.
Na Ujinga wao ndio unaowafanya viongozi wao wautumie kama Mtaji wa kuendelea kuwatawala. Hawajui kuwa Jeuri na Uongozi au Mamlaka zote walizonazo Viongozi wao yanatoka kwako. Hawazijui Haki zao. Hawajui kuwa rasilimali za Taifa lao zinaliwa na watu wachache (1% ) ambao ndio viongizi.
Hawa ni Waoga wanaoogopa hata kutoka usingizi ili wauone mwanga wa kuzifanya akili zao zifanye kazi na kuujua udhalimu wa Viongozi wao.
Hawayajui Maovu ya Viongozi wao. Hawaujui ukweli wa mambo yanayofanywa na Viongozi wao. Hawa ndio "Wajinga ndio waliwao, na wanaliwa na Viongozi kwa ujinga wa wajinga".
5% πΎπππππππ ππππππ ππ πΎππππππππππ 90%
Hawa ndio Walimu, Wanasiasa, Viongozi wa Dini, Wanaharakati, Asasi za Kijamii na Kiraia, Wasanii, watu Maarufu na wenye Ushawishi katika jamii, Wanasheria, Wanazuoni. Wanajua kila kitu kibaya na kizuri kinachofanywa na Viongozi wao. Wameshika Tochi yenye Mwanga (Elimu).
Mwanafalsafa Nguli wa Kiyunani (Kigiriki) Socrates (470-399 B.C) anaulinganisha "Ukweli = Maarifa = Mwanga". Ndio asili ya Msemo, "Elimu ni Mwanga." Hawa wana Maarifa ya kutosha kuhusu kinachoendelea duniani. Kwa vile hawako usingizi, ni rahisi sana kwao kuujua ukweli.
Hili ni kundi ambalo ni Tishio sana kwa Viongozi (1%) kwasababu wanaujua ukweli kuhusu Maovu ya Viongozi. Kutokana kuujua ukweli, wanahangaika kwa kila namna kuwaamsha wale 90% waliolala. Yaani Wanawaelimisha 90% ili watoke usingizi waujue ukweli, wajue kuwa wanaibiwa na Viongozi wao.
Hili ndilo kundi linaloogopwa na Viongozi na Watawala wote waovu duniani. Ndilo kundi linaloongoza kwa kuuawa, kutekwa, kuteswa, kunyanyaswa, kubambikiziwa kesi na kufunguliwa Mashtaka ya Uongo. Ndio hawa ambao wengi wao huitwa wazushi, wachonganishi, wachochezi, waanzisha vurugu, wasiolitakia mema Taifa, nk.
Tabaka lolote Tawala au Utawala wowote wa Kidikteta haujawahi kuwa na Urafiki na hili Kundi la 5% ambao wanaujua ukweli kuhusu Uovu wao. Viongozi wote waovu duniani huwa wanatumia kila namna na njia ovu ya 'kuwanyamazisha' hawa.
Baada ya kukufafanulia na kuelewa, sasa nakuuliza: Wewe upo kwenye kundi gani: Umo miongoni mwa 1% wanaoongoza Dunia, 4% ambao ni Vibaraka wa 1% wanaoongoza dunia au umo miongoni mwa 90% ambao wamelala au wewe ni wale 5% wanaujua ukweli na wanawaamsha 90% waliolala?