Falsafa ya Kiafrika ya Ubuntu inavyoweza kusadia kupambana na ubadhirifu wa mali za Umma Tanzania

Falsafa ya Kiafrika ya Ubuntu inavyoweza kusadia kupambana na ubadhirifu wa mali za Umma Tanzania

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora. Ubuntu ni neno la Kingoni linalotafsirika kwa Kiswahili kama "mtu si mtu bali watu".

Msingi wa falsafa hii ni mtu si mtu bali watu. Katika lugha ya Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu".

Falsafa hii inajikita katika imani ya viuganisho vya umajumui huku kuhamasisha upendo na kupinga ubinafsi na unyonyaji. Jadi ya Nchi za Kiafrika haikutoa nafasi ya unyonyaji (Nyerere,1968).

Ni jambo la kujivunia kwa haki kabisa maisha yanayotawaliwa na falsafa ya Kiafrika kuendelezwa kwa kuwa ni sehemu ya maisha ya Kiafrika.

Nyerere(1968) Hatua yetu ya kwanza lazima iwe kubadili mawazo yetu, turudie tena mawazo yetu ya zamani ya Kiafrika...tusikubali wazuke wanyonyaji hapa kwetu...Maneno hayo licha ya kutamkwa zaidi ya miaka 50 ni kama yanatamkwa tena leo hii ili kulishauri Taifa hili. Kupitia falsafa ya Kiafrika Tanzania inaweza kufanya mambo yafuatayo ili kupambana na ubadhirifu wa mali za Umma;

1.Kutambua kuwa watu , hususani Wananchi huumia sana raslimali zao zinappfanyiwa ubadhirifu ndiyo maana ni vizuri kutambua aina mbalimbali za ubadhirifu na kutafuta njia za kupambana nazo.

2.Kuwapa watu nguvu. Ili kuiakisi falsafa hii katika kupambana na ubadhirifu viongozi wanapaswa kutambua kuwa licha ya kukasimishwa mamlaka kutoka kwa Wananchi bado raia wanapaswa kupewa njia sahihi za kushiriki katika Serikali yao katika kubaini changamoto zinazowakabili, aina mbalimbali za ubadhirifu, kubaini vipaumbele na namna ya kutatua changamoto zao.

3.Kutumia njia ya upashanaji habari. Jamii za Kiafrika zilipashana habari kupitia njia mbalimbali. Falsafa hii ya Ubuntu inahamasisha umuhimu wa Umma kuwa na taarifa kuntu juu ya viuganisho vya utu. Serikali katika zama hizi inapaswa kutumia nguvu yateknolojia kwa Umajumui.

4.Serikali inapaswa kuwekeza kwenye taasisi na sera ili kupata maboresho endelevu ya huduma inayotolewa.

5.Utoaji wa adhabu stahiki kwa wabadhirifu. Falsafa ya Ubuntu licha ya kuhamasisha sana umoja, upendo na utu bado inayosisitiza zaidi katika kutoa adhabu kwa wanakula misingi katika lengo la kutoa fundisho ili kukuza zaidi umoja na ushirikiano. Sharti Serikali itoe adhabu stahiki kwa wabadhirifu ili kutoa fundisho kwa jamii.

6.Serikali inapaswa kupambana a ubadhirifu katika mawanda yote, ndani katika jamii,kitaifa na kimataifa. Tukumbuke falsafa hii haijifungi katika eneo dogo ila inaamini kwa watu wote ni ndugu. Katika falsafa hii Afrika ni moja, Dunia ni moja.

Hivyo basi, tunaweza tukarejelea misingi ya mawazo yetu kutatua changamoto zetu za kila siku huku tukipanua mawanda kwa kujifunza kwa wengine.

Ipo methali ya Kiafrika isemayo ukitaka kutembea haraka tembea pekeyako ila ukitaka kufika mbali tambua na wenzako.

Screenshot_20210410-205717_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom