Falsafa ya ‘Law of Pressure’ inavyoiwezesha CHADEMA kuidhoofisha CCM na kuzidi kuipa wakati mgumu Serikali na Vyombo vya Ulinzi

Kwa jinsi ulivyoandika hii mada kirefu ungetumia huo muda kutafuta pesa ungekuwa milionea
 
CCM hawasomi hizi nadharia za vyuoni wao wanakwenda moja kwa moja kutatua shida za watu wa vijijini kwa kusambaza umeme na ujenzi wa barabara za lami.

Hizi nadharia hakuna mtanzania wa kawaida mwenye muda hata wa kujua zipo wapi, zinaishia humu humu JF na vitabuni zinakotolewa.
 
Yaan unaandika vitu vingi ambavyo havina impact wala ukweli wowote.
Kibaya zaidi nachokiona kikitokea kwa kipindi kifupi kijacho ni endapo pia kama hawa vijana waliotekwa watashindwa kupatikana maana yake nao watakuwa wameuawa. Hiyo maana yake itaibua kuongezeka kwa pressure kubwa kutoka CHADEMA na jumuia ya kimataifa, ukizingatia ya kwamba tayari mauaji ya Kibao yamewazindua wakubwa wa dunia ambao its obvious bado Tanzania hatuna kinga dhidi yao.(WEWE NI MWEHU)
 
Kwa jinsi ulivyoandika hii mada kirefu ungetumia huo muda kutafuta pesa ungekuwa milionea
Kachukua mada nzima kutoka kwenye vitabu na kuhamisha humu JF, ndio wasomi wetu hawa. Hapo unakuta anajidanganya kuwa ameandika kitu cha maana sana Jamii Forum.
 
Waingereza, Wajerumani wapo humu nchini wakiwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya kina aina, hakuna cha maana kitakachotokana na hiyo presha, kwani wenye kutegemewa kuwapa presha viongozi wa serikali ni marafiki zao wenye maslahi mapana ya pamoja.

Ni utoto kuamini kwamba siasa za maandamano zinaweza kuja kuiondoa CCM kwenye umiliki wa dola.
 
200% true Mkuu....!

Ngumu Sana Kwa Kilaza kuelewa huu Uzi...!!!
 
Udhaifu wa CHADEMA ni kushindwa kubadilisha uongozi wa juu na hivyo kuendelea kunasa kwenye tundu lile lile bovu miaka na miaka.

Hizi nadharia siku zote huwa zinakosa mashiko.
 
Kama umeme na maji ingekuwa issue, makaburu wa afrika kusini hadi leo wangekuwa madarakani.
 
Kama umeme na maji ingekuwa issue, makaburu wa afrika kusini hadi leo wangekuwa madarakani.
Unataka kusema CHADEMA wakiingia ikulu haya mauaji yanayoendelea nchini yatakuwa yamefika mwisho?.

Tupa hilo shuka pembeni, simama jinyooshe kumeshakucha.

Hiyo amani ya kweli unaipata ukiwa ndani ya jeneza, dunia haina usawa wala haki.
 
🗑🚮🗑🚮
Jidanganye,
Mzee kama huyu hapa chini ambaye mmeteka mwanaye, pamoja na ndugu zake, jamaa, marafiki, majirani, wanakijiji wenzake, wakazi wa vijiji jirani nk, wanaweza kuelewa hizo ngojera zako ambazo kiuhalisia ni propaganda na uongo mtupu?!!!

View: https://youtu.be/c2R8XUGuhI8?si=Kw5u5JtpaAkqNGJS
 
Umefanya analysis ya hii situation Kwa hali ya juu sana👋👋
 
Hizi ni sehemu ya siasa nyingi ambazo CCM wanazifanya. Kuwatoa ikulu ni kazi nzito. Unapoona kilio cha mzee huyu jua wapo mamilioni kama huyu wanaobadilisha hali zao za maisha kwa kupitia sera za CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…