zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,644
- 3,176
Wale wanaobeza wengine kwa kuwaita MATAGA wanafanya hivyo wakielewa hata maana ya neno MATAGA "Make Tanzania Great Again"?
Taifa lilikuwa linaielekea kubaya hadi 2015, na watu tulitaka mwelekeo mpya wa nchi yetu.
Doctrine ya MATAGA ni kujenga nchi yenye sifa zifuatazo:
Viongozi watakaoweka maslahi ya taifa kwanza, badala ya kuifanya Tanzania shamba la bibi.
Nchi itakayozalisha Made in Tanzania za kutosha, badala ya kujenga uchumi wa kichuuzi.
Nchi itakayojitosheleza kinishati.
Nchi yenye miundombinu bora ya usairishaji wa nchi kavu, majini na angani.
Nchi yenye sauti, kwamba kiongozi wa Tanzania akitamka Afrika na dunia nzima isikie -- kama Nyerere alivyokuwa.
Nchi ya wachapakazi, wazalishaji na inayojitosheleza kichakula na kwa mahitaji mengine ya msingi.
Nchi tajiri, na inayoukataa umaskini akilini hadi kivitendo.
Nchi yenye uthubutu wa kunia na kufanya makubwa.
Ninatazamia siasa za Tanzania kuelekea 2025 zitawagawa watanzania katika makundi haya mawili.
Kundi la kwanza ni kundi linaloamini katika falsafa ya MATAGA, kwamba Tanzania ina potential, na ikithubutu inaweza.
Kundi la pili ni kundi la wanaojikunyata, wanaoamini bila kudra kutoka Washington au Beijing, basi hatuwezi.
Kwa wale mtakaowania 2025 tunarudia kusema tena spirit ya Hayati Magufuli haijafa!