Familia kuongea Lugha 1 ni muhimu sana kwenye mafanikio ya Biashara

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Kuongea Lugha moja ndio moja ya nguzo zinazo wasaidia Wahindi. Wahindi Familia nzima wakikaa huongea Lugha 1 tu. Lugha ninayo zungumzia ni Lugha ya Biashara na si Lugha, Kiswahili au Kichaga au Kisambaaa hapana

WAHINDI
Wahindi biashara anayofanya Baba basi hata watoto ni hiyo hiyo na mama ni hiyo hiyo. Hawa jioni wakikaa wanaweza ongea lugha moja.

Kama Muhindi ana Dilli na Hardware jua kabisa watoto wake na Mke wake nao ni Hardware, hawa wanaweza kaa wakaanza kujadilia bei ya Cement, hawa wanaweza anza kujadili bei ya Nyundo au wafungue sasa kiwanda cha kutengeneza misumari.

Hawa wakiwa Holiday labda wako Serengeti National Park wote wanajadili ishu moja tu Hardware.

Mwaka Jana niliambiwa Tajiri wa Mabasi ya Coast Line alisha fariki, yule Jamaa alikuwa Mwarabu. Baada ya ile taarifa nilivuta Picha ya Basi yake ya Musoma to Arusha kuna wakati Mke wale alikuwa ndio masimamizi wa hiyo route, yaani mke anatoka na Basi Arusha hadi Musoma na anarudi, fikiria yale Mashimo na Vumbi ya Serengeti.

Yule Mama nadhani hakuna asicho jua kuhusu Basi na hata kuhusu fitina zote za Usafiri wa mabasi na nadhani hata Engine anajua kila kitu. Yule mama, natumaini ndio kashika Uongozi na kila kitu kinaenda sawa. Hii ni kwa sababu walikuwa wanaongea Lugha 1. Jioni, wote wanaongea Mabasi, wanajadili waanzishe route ipi kwa sasa.

Kuna pia Wabongo wachache walio fanikiwa kwa hili kwa Mke na Mme na watoto wote kuongea Lugha 1.

MADHARA YA KUONGEA LUGHA TOFAUTI
Hakuna kitu kibaya na kinacho katisha tamaa kama ukute Baba ni Mkulima mkubwa sana ila mama hobby yake ni Urembo, watoto hobby zao wengine ni maduka ya Nguo na wengine ni kazi wamejiriwa. Mzee akiwa nyumbani hana wa kuongea naye kuhusu Kilimo maana mama huko sio Hobby yake.

Hapa mzee akivuta within a month mashamba yanapigwa mnada.

Au Mama ana Hobby ya Ufugaji wa kuku ila mzee hobby yake ni kazi ajira, mnakaa mama anaanzisha mada ya Ufugaji kuku baada ya Dakika kadhaa baba anachomekea kuna nafasi mpya za kazi ngoja niombe.

Biashara nyingi zilizo kufa baada ya waanzilishi kufariki ni kwa sababu ndani ya Familia walikuwa kila mtu na Lugha yake.

Pia kuna Biashara zilizo kufa au mmiliki kufirisika kwa sababu ndani ya Familia hakuna alie kuwa ana muunga mkono maana kila mmoja na Lugha yake.

Hivyo hakuna kitu kizuri kama wote kuwa na Hobby sawa, kwamba kama ni Biashara ya Mabasi basi kuanzia mama hadi watoto wote wanajua mambo ya Mabasi A to Z.

Kama ni Kilimo familia nzima wanajua mambo ya Kilimo A to Z.
Nina ushahidi wa watu walio kuwa wakulima wakubwa na baada ya kufariki watoto wakauza kila kitu hii ni kwa sababu haikuwa hobby yao.

Tuwaige Wahindi na Waarabu kwenye Kuongea Lugha 1 ndani ya Familia



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na hoja yako lakini wengine wameajiriwa navwamewafungulia wake zao biashara. Cha muhimu ni kupeana sapoti. Kuhusu kurithi inategemea kama kuna mtoto ameandaliwa (recession plan) kuchukua hiyo biashara



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada upo sahihi, Kuna mengi ya kujifunza hapaaa
 
hongera kwa somo zuri sana!
 
Ili ufanikiwe vitu kama hivi inabid muoane watu wenye roho nyeupe mambo ya husda sijui wivu na ubinafs visiwepo

Waafrika wengi tuna husda , wivu na ubinafs wako baadhi ya wamama hela yake bora aifiche lakin asiendeleze mradi wa familia kisa ni kaz ya mwanaume

Wako baadhi ya wababa hela yake aitumie kweny starehe lakin ya mwanamke ndo ihudumie familia

Hizi ni baadhi ya changamoto zinazoikumba familia nyingi watu wameoan lakin ni wabinafs hawatanguliz masilah ya familia mbele

Wazaz wengne wakijaaliwa vipato na biashara hawashirikish watoto kwa kigezo cha katafute za kwako nimeshakusomesha hiz ndo zinafanya familia nying za kiafrica ziendelee kuwa maskini

Ni nadra kukuta familia ya kiafrica ikiachiana urithi wa mali kwa zaidi ya vizaz vitatu maana lazma ubinafs uingie plus wivu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes na pia ndo sababu ya Biashara kufa pale Mwanzilishi anapo Fariki, Make walio bakia walikuwa hawana habari na hiyo project
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah ubarikiwe sana kaka kwa somo hakika hizi ndo mada zinazotakiwa kujadiliwa apa Jf kwa kweli ni hii ni mada moto kweli kweli na hili ndo jambo ambalo linatukwamisha waafrika wengi Asante sana inabidi tuanze kulifanyia kazi somo lako thanks mkuu.

Ila naona wadau kama vile wameususa huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…