Familia moja yataka haki itendeke baada ya kifo cha Khamisi Juma Bega (49), bodaboda ambaye alipigwa na polisi hadi kufa

Familia moja yataka haki itendeke baada ya kifo cha Khamisi Juma Bega (49), bodaboda ambaye alipigwa na polisi hadi kufa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Familia moja nchini Kenya yataka haki itendeke baada ya kifo cha Khamisi Juma Bega (49), bodaboda ambaye alipigwa na polisi hadi kufa.

Inadaiwa Khamisi alipigwa na maafisa wa polisi wakishinikiza kufuatwa kwa sheria ya kubaki ndanii kwa kipindi hiki chenye tishio la #Covid19.

Ijumaa, siku ya kwanza ya zuio la kutoka nje, Khamisi alipigiwa simu na mteja wake mjamzito, aliyetarajia kujifungua hivi karibuni. Mjamzito huyo alimuomba Khamisi ampeleke hospitali, ambako alikutwa na mkasa huo.

Ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu usiku alipokuwa akirudi kutoka hospitali, alikutana na maaskri waliokuwa kwenye doria. Inasemekana alipigwa na hakuweza kupatiwa matibabu kwa usiku huo na alipaswa kutulia hata kesho yake, Khamisi alifariki kutokana na majeraha hayo.

Polisi wamekataa madai hayo, kamanda wa Polisi Francis Mguli amesema watachunguza tukio hilo. Wakazi wameomba IGP awaatahadharisha polisi kwenye kutumia nguvu katika kutekeleza agizo.
 
Hiyo familia itasubiri sana, waulize familia za Jacob Juma, Msando, na watu waliouliwa wakati wa vurugu za chaguzi zote za Kenya zilizofanyika kama kuna haki yoyote wamepata, "Kenya not yet Uhuru".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom