kecious Chanila
New Member
- Jun 1, 2023
- 1
- 2
Tunatamani Kila kitu kiwe bora na chenye manufaa, tupate viongozi bora, utawala bora na viongozi wanao wajibika kwenye majukumu yao ipasavyo pasipo kutegea lakini tumesahau kila kitu kizuri kinaandaliwa kwa kutumia nguvu kubwa na gharama kubwa sana ili kuleta faida kubwa pia.
Familia ni muunganiko wa Baba, mama na watoto na ndiyo taasisi pekee yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza na kuandaa viongozi bora tunaowategemea kwa ajili ya utawala bora na uwajibikaji kuanzia kwenye familia na nchi yetu kwa ujumla. Kabla hatujawaangalia watoto, mke na mume ambao ndiyo waunganishi wakubwa wa familia wanalojukumu la kuuishi ukweli na uwazi, utiifu na nidhamu kwao binafsi ili kujenga familia Bora.
Mwanaume analojukumu la kumpenda mkewe, kumjali na kumtunza katika mazingira yote na kwa kufanya hvyo ataepukana na tabia mbaya kama usaliti na unyanyasaji wa kijinsia kwenye familia yake kwanza kabla hatujaangalia jamii kwa ujumla.
Mwanamke kwa upande wake analojukumu la kumheshimu mumewe na kujitiisha kwake akijua kwamba hata angefanya chochote cha kubadilisha yeye kuwa kwenye nafasi ya mwanaume bado hatafikia viwango na nafasi ya kuwa mwanaume. Kila mmoja na amheshimu mwenzake katika nafasi aliyopo ndipo tutaweza kutengeneza na kuandaa utawala bora na viongozi wanaowajibika ipasavyo.
Kitu kikubwa ambacho ni mhimu wazazi wafahamu ni kwamba ni kazi ngumu sana kwa mume na mke kuwaongoza watoto wao katika maadili sahihi wakati wao wenyewe hawayaishi hayo maadili. Watoto hujifunza kwa kuangalia kwa wazazi wao, hata mimi pia nimejifunza kutokana na kuwaona wazazi wangu wanavyotenda wanapokuwa mbele yangu. Mtoto ataheshimu kwa kuona namna ambavyo Baba na mama wanaheshimiana, kadharika ataonesha dharau kama ambavyo wazazi wanaoneshana dharau.
Hapa ndipo penye maarifa wazazi wajue namna ya kuenenda mbele ya watoto wao kwa sababu tabia zao zina athari kubwa kwenye maisha ya watoto wao. Tunao watoto tofauti kwa sababu ya familia tofauti walizotoka, lakini pia tunao viongozi tofauti kutokana na malezi waliokuzwa nayo huko walikotoka.
Baba ndiye mkuu ama kichwa cha familia mwenye wajibu wa kuongoza na kuonesha njia kuanzia kwa mkewe na watoto pia. Kwa nafasi ya Baba pekee ana uwezo wa kuwatengeneza na kuwaandaa watoto kwenye viwango Bora vya kitabia vinavyokubalika katika jamii kama vile uwajibikaji, ukweli, utiifu, uhodari na kujituma, mtoto mwenye tabia hizi tunategemea kwa asilimia kubwa atafaa kuwa kiongozi Bora anaefaa kwenye majukumu yake.
Ni jukumu la Baba kuweka utaratibu unaofaa na kukubalika kijamii ili familia yake uufuate na kuanzia hapo watoto watajifunza kutii na kuheshimu mamlaka iliyo juu yao. Si hivyo tu, Baba anapaswa kila siku kupata muda wa kukaa na watoto ili kuonya, kufundisha, kukosoa na kuadabisha mahali ambapo watoto hawaendi sawasawa kwa kufanya hivyo watoto watajifunza nini kinachofaa kutendeka na kipi wasifanye.
Mama ni mtu wa kwanza kutambua uelekeo na mabadiliko ya tabia ya mtoto kwa ujumla kwa sababu mda wote anakuwa karibu nae hivyo uwezo wake ni mkubwa zaidi katika kuhakikisha mtoto anakua katika malezi Bora kwa kumzuia kufanya yasiyofaa katika jamiii.
Ukweli ni kwamba hakuna kiongozi anaeweza kuwajibika katika nafasi yake wakati kuna migogoro ya kifamilia inaendelea kwenye familia yake, hivyo mambo mazuri yote tunayoyataka yatokee yanapaswa kuanzia kwenye familia zetu kuwa mazuri, hakuna mtu ambae hatoki kwenye familia na kwa namna yoyote ile kila mtu anaguswa endapo jambo lolote baya litatokea kwenye familia mfano ugomvi, mafarakano, kutengana, unyanyasaji, dhuruma na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Kwa mtazamo huo basi wazazi wanalojukumu kubwa la kuwafundisha watoto wao namna ya kukabiliana na majukumu yao siku za usoni, kuwapa kazi za kufanya na kuwaelekeza namna ya kujitegemea, Kwa mfano Leo hii tuna vijana wengi tegemezi kwa sababu ya malezi waliokuzwa nayo, hata kama mtoto anasoma shule ya Bweni anaporudi likizo apewe kazi za kufanya kabla hajarudi shuleni tena hii itamsaidia mtoto kukabiliana na majukumu yake Kila anapopewa kazi za kufanya mahali popote atakapokuwa. Kila usumbufu tunaoupata Leo kutoka Kwa watu wanaotuzunguka ni kwa sababu wazazi wao waliwaacha tu waende wanavyojiskia hata kabla ya umri wa kujiamlia cha kufanya haujafika.
Tunapokuja kuzungumzia suala la uwajibikaji, tukianza na familia yenyewe wazazi ambao ni mke na mume waungane na kuonesha ushirikiano wa kuwalea watoto kwenye maadili sahihi, Baba asimuachie mama pekee kazi ya kulea vilevile mama pia asimuachie Baba pekee kazi ya kuwaadabisha watoto sauti zao zina mamlaka tofauti ya kuonesha na kubadili uelekeo wa tabia ya mtoto na Kwa kufanya hivyo itatusaidia kupata viongozi sahihi wa kutuletea Utawala Bora nchini kwenye taasisi zote.
Haitokei tu kiongozi akawathamini wale anaowaongoza kama alishindwa kuwathamini watu wa familia yake, kiongozi hawezi kuwaheshimu viongozi wenzake kama hakujifunza kuheshimu utawala na mamlaka ya wazazi wake kwenye familia. Sasa tunaweza kuona ni namna gani familia inawajibu mkubwa zaidi katika kuhakikisha tunaupata Utawala Bora tunaoutazamia kwenye uongozi.
Tulipata viongozi bora waliopo na waliopita wenye maadili na uwezo wa kuchambua na kufanya maamzi sahihi Kwa niaba ya jamii nzima kwa sababu familia zao ziliweka juhudi za kuwalea kwenye maadili sahihi yanayokubalika kwenye jamiii. Wazazi wasizae tu na kuwaacha watoto wajilee wenyewe na kufanya kila wanachokiona kwao ni sahihi wajue nafasi yao katika kuharibu ama kutengeneza hatima za watoto wao kwa ajili ya familia na Taifa kwa ujumla ni kubwa zaidi.
Familia inayo nafasi kubwa kuliokoa Taifa na kizazi chenye maadili mabovu yasiyokubalika kabsa na kuleta msawaziko kwenye uongozi na jitihada kubwa zinazotumika na viongozi ili kuboresha maadili kwa kuhakikisha misingi mizuri inawekwa ili kumlinda na kumuandaa mtoto kukabiliana na majukumu yake kwa juhudi na maarifa huku akiheshimu na kushirikiana na wale wanaomzunguka kwa upendo na umoja.
Hatuna nafasi ya kulaumu na kulalamika juu ya uongozi mbaya na Utawala mbovu zaidi sana tunayo nafasi ya kuangalia ni kwa namna gani tunaweza kuandaa kizazi bora kupitia malezi sahihi ili kupata viongozi bora na sahihi tunaowahitaji tukianza na familia, jamii husika na Taifa kwa ujumla. Tutakuwa tumechelewa sana kuona makosa ya kiongozi tayari akiwa kwenye Uongozi, wakati ilikuwepo nafasi ya kumrekebisha bado akiwa kwenye hatua ya familia yake na umri wa kurekebishika.
UTAWALA BORA UNAANZA NA FAMILIA
WANANDOA SAHIHI,WENYE MALEZI SAHIHI, WATOTO SAHIHI WALIOFUNDISHWA NA KUJENGWA KWENYE MALEZI SAHIHI TUSHIRIKIANE KUJENGA FAMILIA BORA ZENYE MAADILI BORA KWA UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI.

Upvote
2