Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,957
1. Familia ya Kenyatta ambayo kitovu chake ni hayati Mzee Jomo Kenyatta, mwanzilishi wa taifa la Kenya na babake rais wa sasa Uhuru Kenyatta, ndiyo tajiri zaidi Kenya.
Ripoti inasema familia ya Kenyatta ina mali ambayo thamani yake ni kati ya $100 milioni na $1 bilioni (KSh9.95 bilioni na KSh99.53 bilioni).
Familia hiyo imewekeza katika sekta karibu zote ikiwemo benki ya Commercial Bank of Africa, hoteli za Heritage, uchimbaji madini, bima, safari za ndege, elimu, kilimo, nyumba na kawi.
Vile vile, wanamiliki maelfu ya ekari za mashamba Kiambu, Endebess, Rumuruti, Nakuru, Naivasha, Nairobi, Pwani na Thika.
2. Familia ya Moi
Familia ya pili ni yake Rais Mstaafu Daniel Arap Moi - Rais wa pili wa Kenya aliyeongoza kwa miaka 24.
Familia hii inakisiwa kuwa na mali ya mabilioni ya pesa ambayo imewekeza ifuatavyo: katika benki mbili za humu nchini, mafuta, bima, hoteli na utalii, habari, utengenezaji bidhaa na safari za ndege.
Pia inamiliki mashamba makubwa na vile vile inasemekana kuwekeza katika elimu, usafiri wa baharini na usafiri wa ndege.
5. Familia ya Odinga
Familia ya tano katika orodha hii ni ya Odinga ambayo kitovu chake ni makamu wa rais wa kwanza wa Kenya, Jaramogi Oginga Odinga.
Ikiongozwa kwa sasa na kigogo wa upinzani CORD, Raila Odinga, familia hiyo imewekeza katika mafuta na gesi, kilimo na utengenezaji bidhaa.
6. Familia ya Biwott
Waziri wa zamani wa KANU aliyekuwa na ushawishi mkubwa, marehemu Nicholas Biwott, alijizolea utajiri unaokisiwa kuwa kati ya $100 milioni na $1 bilioni (KSh9.95 bilioni na KSh99.53 bilioni).
Biwott aliyenawiri wakati wa utawala wa Moi, aliwekeza katika kawi na mafuta na ni mmoja wa wanahisa wakuu wa kampuni ya Kobil. Vile vile, alipenyeza katika uchimbaji madini, teknolojia za mawasiliano, kilimo, benki na nyumba.
7. Familia ya Michuki
Marehemu John Michuki alitambulika kwa kutekeleza sheria kali za kudhibiti sekta ya uchukuzi lakini pia alijua jinsi ya kuunda pesa.

Waziri huyo wa zamani na msimamizi wa utawala wakati wa mkoloni anajivunia utajiri wa kati ya $30 milioni na $100 milioni (KSh2.98 bilioni na KSh9.95 bilioni).
Uwekezaji wake uko katika hoteli ya Windsor Golf and Country Club mjini Kiambu, anamiliki majumba kadha ya kibiashara mjini Nairobi na kilimo.
Wanasiasa wengine matajiri Kenya ni Naibu Rais William Ruto, marehemu Njenga Karume, Harun Mwau na waziri wa zamani Simeon Nyachae ambaye amevuka mpaka na kununua mashamba makubwa nchini Australia, Zimbabwe na Afrika Kusini.