Familia ya Gwajima imemkosea Waziri wa Afya, kiungwana wamtafute wamuombe radhi

Yawezekana uko sahihi hapo kwenye sehemu ya kuharibu ndoa.
Kwenye swala la kudorora au mwitikio mdogo wa watu kuchanjwa ni kosa la mamlaka.
Kutokana na misimamo wa marehemu magufuri, ukifuatiwa na matamko ya mawaziri baadhi yao kama waziri Mkuu,waziri wa afya na naibu wake kuhusu ugonjwa wa Kiroma na chanjo ,ilifaa kabisa waondolewe kwenye nafasi zao kabla ya kupokea chanjo na kuanzisha kampeni kwa watanzania waikubali. Anayoyasema Mchungaji Gwajima leo ndiyo yaliyosemwa na watajwa hapo juu na maneno yao yakapokelewa kwenye akili na mioyo ya watanzania. Ni vigumu sana leo kuyandoa hayo katika akili na mioyo ya watanzania kwa kutumia watu wale wale,hata kama watanzania wanachukuliwa kama wajinga na watu wasio na kumbukumbu. Vinginevyo walitakiwa waombe radhi kwa watanzania, waseme wazi awali tulikosea lakini usahihi wa hali ya korona na chanjo ni huu.
Rais awaondoe hao aweke watu wengine ambao watasema tofauti na hao
 
Niwaombe watanzania,kuna mambo muhimu sana yanayoulizwa watanzania zaidi ya hiyo covd ,chanjo zimeshaletwa ni wajibu wako kuchanjwa. Yapo maswala ambayo yanaumiza unataka ama hutaki,.swala la vifurushi tuliambiwa waziri husika ameunda tume kama sikosei ya itakayokuja na majibu kutokana na kilio cha watanzania, swala la tozo za miamala pia tumeambiwa Rais ameunda tume , mafuta ya kula bei ipo juu sana tukaambiwa serikali inashughulikia ili kupunguza makali. Yote haya hayajapata ufumbuzi. Limeletwa hili la kulipa kodi za majengo pale unaponunua umeme, kuna watu wana vibanda vya biashara, kibanda ambacho hakina hadhi ya nyumba, lakini kwa kuwa kimewekwa umeme unaambiwa ulipe kodi ya jengo. Muda mwingi tunaotumia kujadili malumbano ya familia ya Gwajima hebu tuutumie kuikumbusha serikali ahadi zake kuhusu kero za watanzania.
 
Kumbe huwa unayasikiliza.utaachaje kuelewa kitu kama hujakisikiliza?.mpaka hapa umekuja kuchangia inamaana unamfatilia zaidi
Sina muda wa.kupoteza ndugu yangu. Na taarifa zake sisomagi. Nikiikuta huwa naruka.
 
Binafsi ninaona kama wote wana shida mkuu labda kama unaona waziri ndiye anaepaswa kuheshimiwa pekee. Yale aliyoyasema waziri kwa mchungaji uliyasikia? Kwa kifupi, hao wote ni shida.
 

Inaelekea Gwajima kampa baba yake ukwe wa moja kwa moja lakini kuna mzee Gwajima ambaye ndiyo mkwe wa kweli kafariki mwaka 2019 nasikia tena kwa ugojwa huohuo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…