Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.
Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?
Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.
Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.
Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.
Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.
Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.
Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.
If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.
Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.
Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.
Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.
Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.
Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.
Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.
Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.
Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.
Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.
Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?
Vigumu sana kuamini hilo.
Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.
La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.