Familia yamtia hasira Aslay

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

Msanii muziki wa Bongo Flava, Aslay amesema uwepo wa familia nyuma yake kunampa hasira ya kufanya muziki mzuri.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Natamba’ ameiambia XXL ya Clouds Fm wasanii wote ambao wanafanya muziki kutokana na sababu fulani nyuma yao kama hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kufika mbali.

“Kwanza kabisa sipendi msanii ambaye anavimba, napenda msanii anayefanya kazi kwa kuonyesha mimi nyuma nina watu/familia, kwa watu kama hao huwa nawaheshimu sana kwa sababu huwa na hasira na maisha halafu ukiangalia kazi zao lazima ziwe nzuri mmoja wapo ni mimi” amesema Aslay.

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa anajitahidi kufanya muziki kwa sababu kuna familia inamtazama na licha kujitahidi ana kipaji pia.


Muungwana
 
Mmh anajipaisha sana siku hizi
 
Mimi vilevile nina hasira sana, hasa nikishapiga ulabu.
 
Nina hasira kuna wasenge wananidharau kishenzi
Ilaaaaa muda wao waja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…