Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Familia ya marehemu Mahmoud Ally Hamad Bwato, imeomba msaada kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili iweze kupata hati ya kiwanja chao namba 186039/95, kilichopo Ada Estate, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waadishi wa habari Novemba 25, 2024, Msemaji wa familia na msimamizi wa mirathi, Hassan Mahmoud Ali Bwato, ametoa ombi la familia kwa Rais Samia Suluhu, akilieleza kuwa mgogoro huo umeibuka baada ya mtu aliyedai kuwa amejitokeza kutoa msaada kwa familia hiyo baada ya kifo cha baba yao, Mahmoud Ally Hamad Bwato kumilikisha kiwanja hicho.
Hata hivyo baada ya michakato iliyohusisha ukaguaji wa nyaraka mbalimbali ambazo alikuwa nazo (aliyejimilikisha aridhi hiyo) iligundulika kuwa ni tapeli kutokana na nyaraka za kufoji alizokuwanazo.
Hassan anasema kuwa tangu mwaka 2018, baada ya kikao cha Agosti 24, licha ya kubainika hivyo kutokana na jitihada za baadhi ya viongozi wa Serikali lakini bado hakuna hatua yoyote ya kukabidhiwa hati halali ya kiwanja hicho, badala yake licha ya kurejeshwa kwenye makazi hayo lakini hawana hati jambo ambalo linaendelea kuwapa hofu.
Kutokana na maelezo ya Msemaji huyo wa familia inaonesha hati ya kiwanja hicho ilishikiliwa na Mohamed Ikbar Haji, maarufu kwa jina la "Bagdad", ambaye anadaiwa kuwa na nia ya kupora ardhi hiyo.
"Familia yetu imekuwa ikiteseka kwa miaka mingi, na hadi leo bado hatujapata hati halali ya kiwanja chetu, licha ya hatua zilizochukuliwa na viongozi mbalimbali ili kuthibitisha ukweli wa hali hii. Tunamwomba Rais Samia Suluhu Hassan kutusaidia kupata haki yetu," alisema Hassan Mahmoud.
Familia hiyo inasisitiza kuwa hatua zote zimebainisha kuwa hati inayoshikiliwa na Mohamed Ikbar Haji ni feki, na inatakiwa irejeshwe kwa familia ili kurejesha umiliki wao halali kama ilivyokubaliwa katika maamuzi ya Agosti 24, 2018.
Inaelezwa kwamba swala hilo lilipita kwenye hatua mbalimbali za uamuzi na kufanya mtuhumiwa kukamatwa na kuonesha nyaraka ambazo baada ya kukaguliwa ilibainika zilizikuwa za kufoji, ikiwemo kutumia Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa feki pamoja na 'Askari feki'.