Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Kijana huyo, Peter Charles (21), mkazi wa kata ya Daraja Mbili jijini Arusha, alidai kupigwa hadi kuvunjwa mguu na askari polisi, akimlazimisha kukiri kosa la kujihusisha na kucheza kamari.
Mei 29, 2024 saa moja usiku, wakiwa watatu nyumbani kwa mmoja wa rafiki yao wakitazama runinga, askari waligonga mlango na kuingia, wakajitambulisha kuwa wao ni askari, wakawabeba kuwaingiza kwenye gari walilokuja nalo.
Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao, leo Septemba 18, 2024, walezi wa kijana huyo, wamesema tangu kutokea kwa tukio hilo, hakuna hatua zilizochukuliwa kwa mtuhumiwa, ikiwemo kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema bado suala hilo linashughulikiwa katika hatua za awali na likikamilika hatua za kimahakama zitafuata.
“Tunashughulikia, bado liko ngazi za chini na likikamilika litafikishwa ngazi ya kimahakama, hivyo subirini tu,” amesema Kamanda Masejo.
Soma Pia:
- Arusha: Afisa Upelelezi Omary Mahita akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia
- Aliyedai kuvunjwa mguu na kigogo wa Polisi Arusha, adai kutishiwa maisha
Bibi wa kijana huyo, Getrude Mollel (61) ameiomba Serikali kuchukua hatua za kisheria, ili mjukuu wake apate haki na pia iwe fundisho kwa wengine.