Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
"FAMILY ECONOMY" TAJIRISHA FAMILIA YAKO.
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Nafunga mwaka 2020 na Kuufungua mwaka 2021 Kwa makala hii. Bila shaka itakuwa sehemu bora katika mapito ya maisha yako. Ni furaha kwangu ikiwa makala hii itakusaidia katika mwaka unaoanza.
Niite Taikon wa Fasihi, Mwana kutoka Nyota ya Tibeli. nyota yenye Mbawa mbili kama tai Izungukayo katika vizio vya nyota ya Sabeli.
Basi wala sikusudii kuwachosha, nitasema kwa kifupi ili wale wadhaifu wasinione mbaya, tena sitaki wajione ni wavivu na wazembe bali wajionee fahari katika jumbe hii.
Haya nianze sasa;
Kila mtu duniani hutafuta maisha mazuri, ni ndoto ya kila mwanadamu kuwa na familia bora, familia yenye furaha, amani, upendo, utulivu na mafanikio ya kila namna. Watu wengi wamekuwa wakiniuliza namna bora ya kuwa na maisha bora, wengine imewachukua na kuwagharimu kusafiri umbali mrefu kuja kuniona na kunitembelea kusudi tupige soga na mijadala ya namna ya kuwa na maisha bora. Wapo wanaonipigia simu, kunitumia jumbe kwenye WhatsApp, na messenger wakilenga zaidi kupata suluhu ya maisha bora. Kwa namna hiyo, ndio maana imenipelekea kuandika jumbe hii.
Maisha bora ni kuwa na familia bora, familia bora ni kuwa na Baba bora, Baba bora bora ni kuwa na Mama bora. Mama bora ni kuwa na watoto bora. Hii ni kanuni namba moja ya Family economy.
Ili familia iwe bora hakiangaliwi kipato au utajiri wa kushikika baina ya wanafamilia, kinachoangaliwa ni mshuko na mpando wa uchumi ndani ya Familia.
Naweza kumchanganya mtu fulani hapa, sikusudii kufanya hivyo. Nafikiri nieleze baadhi ya istilahi ambazo zinaweza zua utata kwa kifikra kwa baadhi ya watu.
FAMILY ECONOMY au Uchumi-familia
Ni yale mambo yote ambayo yanazunguka wanafamilia ambayo yakitumiwa vizuri yanaweza kuzalisha faida ndani ya familia bila kuathiri mahusiano ndani ya familia. Mambo hayo ni kama vile Nguvu, akili, vipaji au karama, ujuzi na maarifa, uzuri, sauti na lugha, Mamlaka na udhaifu, Imani, Siri, uaminifu, Ulinzi, upelelezi au udadisi, mvuto, utunzaji, maono, uthubutu miongoni mwa mambo mengine. Mambo hayo ndio huitwa Family Economy ambayo ndio msingi bora wa familia yoyote kuwa bora. Hii ni kwa Mujibu wangu mimi Taikon.
Katika familia kila mwana familia anajambo lake ambalo ni muhimu katika kuifanya familia iwe bora. Kila mwanafamilia ana set yake ya Family economy.
Kwa mfano,
Baba, ana Nguvu, Akili, Karama au kipaji, ujuzi na maaarifa, Mamlaka, ulinzi, siri maono kuliko Mama
Mama ana uzuri, sauti, upelelezi na udadisi, mvuto na ushawishi, kuliko Baba
Watoto wana ubunifu, maono, karama na vipaji, udhaifu, imani, udadisi, uthubutu kuliko Baba na Mama.
Mambo hayo ndio huzalisha mambo yanayoonekana kama utajiri ndani ya familia, jamii, taifa na dunia kwa ujumla. Kupitia mambo hayo familia hupata utajiri wa pesa, majumba, wakati kitaifa nchi hupata utajiri, maendeleo, sayansi na teknolojia, ustaarabu, n.k.
Uchumi wa familia ili uwe imara ni lazima uwe katika muundo huu'
A: Mshuko wa uchumi
BABA
^
MAMA
^
WATOTO
Mshuko wa Uchumi
Yaani Uchumi unatoka kwa Baba kisha unaenda kwa Mama na mwisho unamalizikia kwa Watoto. Hii tafsri yake ni kuwa Baba/ mwanaume ni lazima awe na set nyingi za Family economy kuliko Mama/mwanamke ambaye hapa ni mke wake(Kumbuka hatuzungumzii pesa, wala magari, wala majumba kwani haya ni matokoe ya set za family economy). Mwanaume ni lazima awe na set muhimu za famly economy ambazo ni Akili, nguvu, uthubutu, ubunifu, muono, kipaji/karama na mamlaka. Mambo haya ni lazima mwanaume amzidi mke wake. Kama wewe ni mwanaume fanya ufanyavyo lakini lazima umzidi mkeo mambo hayo saba. Bahati nzuri nature imewapa wanaume wengi mambo hayo. Wanaume wengi wana akili, nguvu na vipaji kuliko wanawake, uthubutu, ubunifu, muono na mamlaka kuliko wanawake.
Mama anapaswa awe na uaminifu, busara, mtunzaji, mzuri, upendo na mambo yote laini laini
B: Mpando wa Kiuchumi
MAMA
^
BABA
^
WATOTO
Mpando wa Kiuchumi
Ni ile hali seti zote muhimu za family economy zinamilikiwa na Mama, yaani Mama anaakili, nguvu, mamlaka na kipaji ndani ya familia. Familia hii huweza kuonekana kwa nje na watu kuwa imeendelea kiuchumi na kutajirika lakini kwa ndani yaani wanafamilia wakawa wanasumbuana wenyewe kwa wenyewe.
Hii wanawake wachache wanayo, ila wengi bado sana kutokana na nature ambavyo katika mgawanyo wa set za family economy bado mwanaume kapewa seti muhimu sana hivyo ni ana nafasi ya kufanya vizuri kuliko mwanamke.
Mwanaume kuwa na seti peke yake hawezi kujitegemea bila kuishi na mwanamke wakashirikiana kwa seti zilizobakia ambazo hana. Ili maisha yawe na maana na yakamilika kwa binadamua basi sharti mwanaume na mwanamke waungane yaani wawe familia, mume na Mke.
Hakuna ambaye ni bora kuliko mwenzake licha ya kuwa mwanaume anamzidi mwanamke katika set za family economy kwa sehemu kubwa na kwa wanaume wengi sio wote.
Watu wengi wanatafuta pesa na utajiri kwa kujitaabisha, kujitesa na kuhangaika usiku na mchana bila kukoma. Wapo wachache ambao wamebahatika kufanikiwa kupata pesa wao kama wao bila kuwashirikisha wake au waume zao. Lakini jambo hili huwa na athari pale wanapooa au kuolewa, kwani ni rahisi kufilisika na kurudi nyuma unapoolewa au kuoa ukiwa tayari unautajiri wa pesa kama utampata mtu ambaye hawezi kutumia set zake za family economy kuboost utajiri alioukuta.
Utajiri wa mtu au wa familia haupo nje kama watu wanavyoona na kufikiri. Utajiri wa mtu au wa familia upo ndani ya mtu au wanafamilia wenyewe. Utajiri wa mtu au familia sio kumiliki majumba, magari, au mali za namna yoyote ile. Utajiri wa familia ni ule uwezo wa kutumia set za family economy katika kuzalisha faida ndani ya familia au jamii. Mtu au familia ambayo ni tajiri na ambayo wanajua kutumia set za family economy hata uwafilisi majumba, magari na mali zao zote lakini ukawaacha hai basi ndani ya miaka saba watarudi katika hali yao ya kwanza. Hii ni kwa sababu utajiri wao haukuwa kwenye magari, majumba, au mali zinazoonekana.
Mbinu muhimu ya kuharibu familia bora na yenye utajiri wa ndani ni kuivuruga kwa kuwatenganisha kati ya mume na mke wake hapo utaweza kuvuruga utajiri wa mtu au familia husika.
Ili familia iwe tajiri au bora basi ni lazima wanafamilia wote waweze kutumia set zao za family economy katika kuzalisha mali kama ifuatavyo;
Mwanaume
1. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili yake kwa kiwango cha juu kama sio cha mwisho katika kuzalisha faida bila kuathiri familia yake
2. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili yake kwa kiwango cha juu katika kumtawala, kumtunza, kumpenda, na kumlinda mke wake. Kwa maanda mwanamke anahitaji mambo manne ambayo ni kutawaliwa, kutunzwa, kupendwa na kulindwa kutoka kwa mwanaume. Na yote yafanyike kwa akili.
3. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili yake kuona, na kubashiri mambo yanayokuja na yatakayotokea kwenye familia yake iwe leo, kesho au hata miaka kumi ijayo na aweze kujiandaa kukabiliana na yanayokuja. Kwani mwanaume hapaswi kusema maisha ni bahati, na ni aibu kwa mwanaume kusema hakujui kuwa itakuwa hivi au vile.
4. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia Akili yake kujua ni wakati gani atumie akili, nguvu au rasilimali yoyote na wakati gani hapaswi kutumia.
5. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili yake kujua kila mtu anayemzunguka, anayezunguka familia yake na sababu ya watu hao kutokea kwa muda huo, awe na uwezo wa kubashiri nani atakuja kesho kwenye mzunguko wa maisha yake na nani ataondoka au atamsaliti kesho.
6. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili na nguvu alizonazo kuchuma mali kwenye mazingira yanayomzunguka ili aipatie familia utajiri
7. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili na nguvu kupigana kwa mwili au kutumia silaha kulinda na kuokoa familia yake. Mwanaume lazima ajue ngumi, kupiga na kujihami.
8. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili kupata taarifa kabla tukio halijamgusa yeye au familia yake.
9. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili, karama, kipaji kumfurahisha mke wake na watoto
10. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia akili, kipaji, na ubunifu katika kuzalisha mali ndani ya familia
11. Mwanaume awe na uwezo wa kuthubutu kufanya jambo lolote atakaloona lina tija kwake na familia yake. Mwanaume hapaswi kuwa muoga. Athubutu kwa akili.
12. Mwanaume awe na uwezo wa kupuuzia mambo ambayo anayaona yapo chini ya mke wake
13. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia nguvu na mamlaka yake kumdhuru, kumuangamiza yeyote ambaye atahatarisha usalama wa familia yake.
14. Mwanaume awe na uwezo wa kumfanya mke wake ajione yeye ndiye mwanamke bora zaidi kuliko wengine duniani.
15. Mwanaume awe na uwezo wa kumfundisha mke wake kumtii, kumheshimu na kumsikiliza kwa manufaa ya familia
16. Mwanaume awe na uwezo wa kumfundisha mke wake Mungu wa kweli na imani thabiti ya familia
17. Mwanaume awe na uwezo wa kutumia nguvu na akili katika kutoa hukumu na adhabu za haki ndani ya familia.
Mwanamke
1. Mwanamke awe na uwezo wa kutumia sauti yake kumtuliza, kumfariji, kumhamasisha mume wake kuzalisha mali
2. Mwanamek awe na uwezo wa kutumia uzuri wake kumpumbaza mume wake asione wanawake wengine walio duniani
3. Mwanamke awe na uwezo wa kutumia ulimi wake kupata taarifa nyeti zitakazo iwezesha familia yake bila kuiathiri
4. Mwanamke awe na uwezo wa kutumia mwili wake kuilinda nyumba yake pale inapoingia hatarini kumpumbaza adui na kumuangamiza bila kutoa penzi.
5. Mwanamke awe na uwezo wa kutumia sauti yake kujenga maadili ya watoto na kuwatiisha kwa baba na jamii
6. Mwanamke awe na uwezo wa kutumia sauti yake kuwashawishi watoto watumia muundo wa mshuko wa uchumi kwani ndio hujenga heshima kwa Baba na familia kwa ujumla.
7. Mwanamke awe na uwezo wa kuiga mazuri yote ya mume wake na kuyafanya bila kumtegemea ili siku Baba akiwa hayupo iwe kwa kusafiri, kuumwa au kufa basi aweze kuendesha familia pasipo shida yoyote au pasipo kuathiri heshima ya familia.
8. Mwanamke awe na uwezo wa kutumia vipaji vya kike kuzalisha mali ndani ya familia kwa kusaidiana na mume wake.
9. Mwanamke awe na uwezo wa kumuelewa mume wake anataka nini na nini hataki ndani ya familia yake
10. Mwanamke awe na uwezo wa kufundisha watoto wake na mumewe dira na malengo ya familia,
11. Mwanamke awe na uwezo wa kuwafundisha watoto kujitegemea wao wenyewe na sio kutegemea wazazi au mtu yeyote yule. Hapa mwanamke awe mfano kwa kujishughulisha kwa shughuli ndogo ndogo, na sio afundishe watoto kujitegemea wakati yeye mwenyewe ni mama wa nyumbani anamtegemea mume wake.
12. Mwanamke awe na uwezo wa kuwafundisha watoto Mungu wa kweli na imani ya familia
13. Mwanamke awe na uwezo wa kuwafundisha watoto wake upendo kwa kumpenda na kumtii Mume wake kwani mwanamke asiyempenda mume wake kamwe hawezi wafundisha watoto wake kupendana. Zaidi ya kufundisha kwa maneno na vitendo chuki atakayoionyesha kwa mume wake mbele ya watoto
BABA NA MAMA
1. Wote wajifunze kupeana na kuachiana majukumu ikiwa yapo ndani ya uweza wa mmoja wao. Kama itaonekana mmoja anashindwa basi mwingine amsaidie. Kwa mfano mambo ya Baba afanye Baba na mambo ya Mama afanye mama pasipo kuingiliana isipokuwa kwa sababu maalumu.
2. Wote wawe na uwezo wa kushirikiana kwa kila jambo liwe nzuri au liwe baya, lakini wajifunze kupeana taarifa kabla jambo halijafanyika ili wajadiliana kama wafanye au laa. Pawe na ushirikishwaji.
3. Wote wazalishe mali kila mmoja kulingana na set zake za family economy na faida iletwe nyumbani. Kuzalisha mali ni jukumu la Wote wawili, Baba na Mama. Kumuachia mmoja ni kutengeneza unyonyaji, utegemezi na magomvi yasiyotarajiwa. Haijalishi nani atazalisha sana lakini kila mmoja aheshimu mchango wa mwenzake. Napendekeza ushirikiano baina ya Baba na mama katika kuzalisha mali. Isiwepo mali ya Baba wala isiwepo mali ya Mama. Bali ziwepo mali zenu/zetu. Hii itaepusha usaliti na ubinafsi huko mbeleni.
4. Wote wasahau kwao. Baba asikumbuke kwao, na mama asikumbuke kwao. Muwe na kwenu. Kuepusha migogoro ya kindugu. Saidieni ndugu kama binadamu wengine. Musiwape nafasi sana. Kuwapa wazazi iwe wa mke au mume nafasi ndani ya familia yako ni kupasua familia yako mwenyewe. Napendekeza, liwepo fungu la nane la mali mtakazochuma kwa habari ya faida ambazo mtawapa hao wazazi lakini wasione kuwa ni lazima ili kuepusha lawama. Hii itawafanya na ninyi mjiandae na uzee kusudi msiwategemee watoto wenu huko baadaye bali wao ndio wawategemee ninnyi kama wazazi wao.
5. Mtumie umoja kwa kila kitu. Penda kusema tumeamua, tumepanga, tunataka, kumaanisha upo wewe na mke wako au wewe na mume wako. Mali zetu, gari letu, shamba letu, hii itaondoa ubinafsi miongoni mwenu. Itasaidia hata mmoja wenu asipokuwepo hatapata shida. Lakini kuigawa familia mkiwa wote ni kujenga nafasi ya adui kuwagawanya. Mfano wababa husema; Sitaki ujinga kwenye nyumba yangu, nitakufukuza uende kwenu hapa sio kwako, unanizuia kuingia kwenye nyumba yangu, hii inatengeneza ubinfasi na mpasuko ndani ya familia. Pia inatengeneza mazingira ambayo hata Mume akifa ndugu za mume wakija husema hii nyumba au mali ni ya mtoto wetu. Lakini kama wangezoea kusikia kwa ndugu yao hivi; tumejenga nyumba, nyumba yetu, kampuni yetu, n.k basi kisaikolojia wangeshadhurika na ingewawia ngumu siku mmoja akiwa hayupo.
Wamama nanyi muache kusema mtoto wangu, bali sema mtoto wetu, kwenye familia ogopa kubinafsisha kitu chochote. Bali kifamilisha kiwe mali ya familia yaani wewe, mumeo na watoto. Hii hujenga unity na upendo wa kifamilia
Nimalize kwa kusema, Kwa Heri mwaka 2020, na Karibu mwaka 2021
Nawatakia Utajiri mwema katika familia zenu. Pole na Hongera kwa kusoma makala ndefu
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam