Fani gani itamfaa huyu mdogo wangu,,ana ulemavu wa jicho moja!

Fani gani itamfaa huyu mdogo wangu,,ana ulemavu wa jicho moja!

KIRIKIOU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2014
Posts
241
Reaction score
57
NDUGU ZANGU NISAIDIENI ILI NIMSHAURI MDOGO WANGU,,,YEYE ANAPENDA UDAKTARI, SASA SIJAJUA HIYO FANI NA TATIZO LAKE ATAMUDU AU ASOMEE NINI. KAMALIZA MWAKA JANA SIX,, HAKUWEZA KWENDA CHUO MWAKA JANA, KWA SABABU YA AJALI YA PIKIKPKI ILIYOMPELEKEA UPOFU JICHO LAKE LA KUSHOTO..!matokeo ACSEE 2013(PCB)(CBB)
 
Udaktari mbona atauweza tu mkuu,mwache atimize ndoto zake bana.
 
Khaaaa!kaka hiyo ni hazina kabisa ya taifa mwombee vyuo vya afya hata utaalam wa maabara jicho si tatizo mkuu,hilo moja linalo ona linatosha kabisa mbona kuna wasio ona kabisa na ni watumishi waadilifu kabisa wa umma !? Hapana kiongozi mtendee haki ya ndoto yake.mpe pole sana pia.
 
NDUGU ZANGU NISAIDIENI ILI NIMSHAURI MDOGO WANGU,,,YEYE ANAPENDA UDAKTARI, SASA SIJAJUA HIYO FANI NA TATIZO LAKE ATAMUDU AU ASOMEE NINI. KAMALIZA MWAKA JANA SIX,, HAKUWEZA KWENDA CHUO MWAKA JANA, KWA SABABU YA AJALI YA PIKIKPKI ILIYOMPELEKEA UPOFU JICHO LAKE LA KUSHOTO..!matokeo ACSEE 2013(PCB)(CBB)

yasiyowezekana kwa binadamu kwa Mungu yanawezekana, kwa upande wangu naona Udaktari ataumudu.
 
Sina hakika sana. Ila fomu za kuthibitisha uzima wa mtu hutumika kama vigezo vya kudahiliwa. Hapa Tanzania sijawahi ona wenye ulemavu wa macho kwenye mambo haya. Ila vema ajaribu anaweza kuwa wa kwanza.

Kuna mambo mengi kwenye shule yanayohitaji macho yawe fit sasa labda usumbufu kwa vile huo ulemavu si wa muda mrefu na inawezekana bado hajaweza vizuri kutumia hilo jicho moja.

Hapo kwa uhakika kabisa hata akiwa daktari wa kawaida hataweza kujiendeleza kuwa daktari wa macho maana hata wenye macho mawili kuna vigezo vya macho wanavyokosa na hawaruhusiwi kusomea huo udaktari.
 
Mwache atimize ndoto yake
 
Back
Top Bottom