Heshima kwenu wanajukwaa
Wahenga waliposema ukubwa ni jalala hawakukosea, walikuwa sahihi kabisa
Niko na wadogo zangu wa kike hapa baada ya kumaliza kidato cha nne hawakufanikiwa kufanya vizuri. Kama mjuavyo jamii imetuaminisha ili ufanikiwe lazima usome upate kazi nzuri hivyo wakajaribu bahati zao tena kwa ku reseat. Hata hivyo hawakuambulia chochote tena
Kwa vile nafahamu uwezo wao kwa masomo haya ya darasani na pia kwa vile nafahamu si lazima kupitia mlango mmoja tu wa mafanikio, ikabidi niwape moyo na kuwashauri watafute fani wanazozipenda
Wote wawili wanaonyesha kutaka ushonaji. Najua ni kwasababu ni wasichana na hawajaona option nyingine. Nami nimejaribu kutafuta fani nyingine naona kichwa kinauma tu
Sido wanafundisha ujuzi wao kwa muda mfupi sana na wamejikita zaidi kwenye usindikaji wa vyakula. Nimejaribu kufuatilia naona wanaendesha mafunzo yao kikanda kwa wiki moja moja tu kitu ambacho kwa begginer ni ngumu ku catch-up
Nakuja kwenu kuomba ushauri kwanza wa fani inayoweza kumsaidia mtoto wa kike kujiajiri na akiweka juhudi atafanikiwa
Na pili kwa yeyeto anayefahamu vikundi au Taasisi zinazoendesha mafunzo ya fani mbalimbali kwa watoto wa kike mbali na VETA na SIDO (VETA interview zao sio rafiki sana hata sijui kwanini mfumo wetu wa elimu unalazimisha haya)
Hata hivyo nitashukuru kupewa mawazo mengine hata nje ya haya
Msaada wenu tahadhari