Fani ya ku-operate mitambo mikubwa inalipa?

Fani ya ku-operate mitambo mikubwa inalipa?

kindoki

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2018
Posts
213
Reaction score
218
Wadau, Ivi fani ya ku operate mitambo mikubwa kama bulldozer, grader, forklift, na mingine HEAVY EQUIPMENT inalipa vizuri?

Chuo chao kipo wapi, mwenye kujua utamu wa fani hii anisaidie tafadhali wakuu.
 
Fork lift unaweza kuisoma chuo cha taifa cha usafirishaji NIT Dar na Chuo cha Bandari Kurasini Dar kuna forklift,front end loader,winch,crane nk.Kwa taarifa zaidi ingia Google visearch vyuo husika hapo juu.
 
Kwanza kwako wewe ukisema malipo mazuri ni kuanzia pesa ngapi?

Ukijibu hilo then ndio tutaendelea na mjadala
 
Mitambo ipi ina market nikaisomee
 
Fork lift unaweza kuisoma chuo cha taifa cha usafirishaji NIT Dar na Chuo cha Bandari Kurasini Dar kuna forklift,front end loader,winch,crane nk.Kwa taarifa zaidi ingia Google visearch vyuo husika hapo juu.
Ivi kwa nyakati izi mitambo ipi ndio inaweza kunipa dili nzur, nataka nichague mitambo ambayo marketable
 
Ivi kwa nyakati izi mitambo ipi ndio inaweza kunipa dili nzur, nataka nichague mitambo ambayo marketable
Kajifunze:-
1. Grader
2. Excavator
3. Mobile Crane
4. Tower Crane
 
Wadau, Ivi fani ya ku operate mitambo mikubwa kama bulldozer,grader, focal lift, na mingine HEAVY EQUIPMENT inalipa vizuri? Chuo chao kipo wapi, mwenye kujua utamu wa fani hii anisaidie tafadhali wakuu
Kwa Awamu hii ambayo imejikita katika Ujenzi / Miundombibu inalipa, ila kwa ninaowajua wengi Wao hiyo hiyo Mitambo imewapeleka Udongoni.
 
Kajifunze:-
1. Grader
2. Excavator
3. Mobile Crane
4. Tower Crane
Mimi nashauri asomee hiyo namba 3 na 4 angalau anaweza kubahatisha kazi kwenye kampuni za logistics akapata maisha.
Hizo grader na excavator wamejazana wengi sana mitaani na tatizo lingine hizo kazi za ujenzi nyingi zinashikiliwa na wachina ambapo hata ukiipata hiyo kazi malipo yake ni duni sana.

Nakumbuka miaka ya nyuma kuna mabrother fulani walikuwa ndio fani yao walikuwa wanakula pesa sana enzi za JK kurudi nyuma,maana walikuwa wakienda site kwenye mradi hawakosi mshahara wa laki 8 na allowance elfu 50 kila siku.
Lakini siku hizi kazi nyingi ni za wachina ukipata mshahara wa laki 4 kachinje kuku.
 
Back
Top Bottom