Fanya haya ili Kuzuia Ajali Jikoni

Fanya haya ili Kuzuia Ajali Jikoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Ajali nyingi zinaweza kutokea jikoni usipokuwa makini. Mambo yafuatayo yatakusaidia kuzuia ajali unapopika na unapokuwa jikoni. Ajali zinazotokea mara kwa mara jikoni ni kuungua, kujikata na vitu mablimbali au kunaguka kutokana na kukanyaga maji na kuteleza.

Mbinu za kuzuia kuungua
  • Unapotoa sufuria au tray kwenye oveni tumia kitambaa kikavu na kikibwa ili kuepuka kuungua mikono/ viganja.
  • Mikono / mishikio ya sufuria na vikaangio ielekezwe upande wa ukutani ili kuepuka mtu kuisukuma kwa bahati mbaya na kuanguka au mtoto kuivuta kwa urahisi na kuleta madhara.
  • Usiache sufuria yenye kitu cha moto kwenye meza ya jikoni na kuondoka. Kama inabidi uondoke na kuiacha basi hakikisha kila anayetumia jiko anafahamu kuwa kuna kitu cha moto na kiwekwe mbali na mahali ambapo watoto wanaweza kufikia.
  • Kama jiko haulitumii ni vyema likazimwa kama ni gesi zima mtungi na kama ni umeme zima ukutani.
  • Ukitumia ‘deep frier’ kukaangia ndizi au viazi basi toa kikaangio ka uweke viazi au ndizi zako pembeni ndipo uweke kwenye mafuta kuzuia kuungua baada ya mafuta kuruka utakapoweka moja kwa moja.

Kuzuia Kujikata
  • Visu na vitu vyote vyenye nja kali vihifadhiwe mahali salama mbali na watoto pale unapokuwa havitumiki.
  • Mikono ya visu iwe imara na isiyopasuka wala kuvunjika.
  • Unapokatakata mboga uwe mwangalifu ili kuepuka kujikata.
  • Unaposafisha chombo chenye ncha kali chukua tahadhari kulinda mikono na vidole vyako.

Kwa Ujumla
  • Usipendelee kuvaa nguo zenye mikono mirefu na mipana unapokuwa jikoni maana nirahisi kukusababishia ajali.
  • Watoto wadogo wawe mbali na jiko hasa unapokuwa unapika.
  • Panga jiko lako vizuri na kila kifaa kiwe mahali pake ili kuepuka hatari zaidi.
  • Sakafu ya jiko lako iwe kavu mara zote kuepuka kuteleza na kuanguka.

Ubarikiwe!

From women of Christ
 
Nimekupenda bure
 
Aise kuanzia leo nitakuwa makini zaidi.
 
Back
Top Bottom