Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
NAMNA YA KULINDA NYWILA (PASSWORD) YAKO
1) Usitumie Nywila (Password) moja kwenye kurasa zako zote za Mitandao ya Kijamii. Hakikisha kila mtandao unatumia #Password yake
2) Hakikisha Nywila yako ina jumla ya herufi/alama zisizopungua 16 au na zaidi (Mfano: M1m1$%678abc@£+#)
3) Usitumie maneno ya kwenye Kamusi kama nywila yako. Na usiruhusu kivinjari chako (Web browsers mfano Chrome, Opera, Firefox, Brave n.k) kuhifadhi nywila yako
4) Usitumie jina la ndugu, Mtoto au Mzazi wako au Wanyama (mfano Mbwa, Paka etc), mwaka wa kuzaliwa au namba ya simu kama nywila yako. Ni rahisi Mtu kuhisi na kukufanyia udukuzi