Fanya haya kupata faida kwenye hisa

Fanya haya kupata faida kwenye hisa

Mwakawasila

Member
Joined
Oct 23, 2024
Posts
23
Reaction score
20
Kunufaika na hisa (au uwekezaji katika soko la hisa) kunahitaji kuelewa jinsi zinavyofanya kazi na kuwekeza kwa busara.

Hisa ni umiliki wa sehemu ndogo ya kampuni, na unaponunua hisa unakuwa mshirika wa kampuni hiyo. Hapa ni njia za kufaidika na hisa:

1. Faida Kutokana na Ongezeko la Thamani ya Hisa Mfano CRDB iliingia sokoni ikiwa chini ya 100 Leo ni 670

Unaponunua hisa kwa bei ya chini na kuziuza kwa bei ya juu baadaye, unapata faida inayojulikana kama capital gain.

Mfano: Ukinunua hisa kwa shilingi 100 na baada ya muda thamani yake ikapanda hadi shilingi 150, faida yako ni shilingi 50 kwa kila hisa.


2.kununua HISA zikiwa bei ya chini na kuuza bei ikipanda

Hii ni Kila siku mfano CRDB mwezi wa 1 na wapili ilishuka Hadi 460 lakini Leo ni 670

3. Kupata Mgawo wa Faida (Dividend)

Kampuni nyingi hugawa sehemu ya faida yao kwa wanahisa kila mwaka au kwa vipindi maalum. Dividendi ni malipo unayopokea bila kuuza hisa zako.

Mfano: Kampuni ikitangaza divident ya shilingi 5 kwa kila hisa na unamiliki hisa 100, utapokea shilingi 500.


3. Umiliki wa Kampuni

Unapomiliki hisa, unakuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni na unaweza kushiriki kwenye maamuzi, kama vile kupiga kura katika mikutano ya wanahisa.

4. Uwekezaji wa Muda Mrefu

Hisa hutoa nafasi ya kukuza mtaji wako kwa muda mrefu kutokana na kuongezeka kwa thamani ya kampuni.

Kampuni kubwa zenye historia nzuri ya utendaji (blue-chip companies) zinaweza kukupatia faida kubwa endapo utawekeza kwa muda mrefu.


Na UKIMILIKI HISA Usikae ni muhimu kucheza kama game

Kuwa makini HISA zunaposhuka
Kuwa makini kujua Gawio linagawiwa lini

Kuna kitu kinaitwa CUM DIVIDEND period ni muda ambao ukinunua hisa unapewa GAWIO
Unaweza kupewa hata mwezi

Mfano AFRIPRISE CUM DIVIDEND PERIOD Ilikuwa 30 September Hadi 18 October 2024

Alafu Kuna hii EX-DIVIDEND PERIOD
ukinunua hisa hiki kipindi HUPATI Gawio
Ukinunua hapa utapata Gawio mwakani

Ni baada ya CUM DIVIDEND PERIOD kuisha
Ukinunua

Kwa hiyo sasa Kuna watu hawawekezi Hela zao muda wote anasubiri kipindi Cha CUM DIVIDEND ananunua baada ya kupata Gawio anauza HISA

Kama Hujasave namba yangu nicheki nikusave

Naweka masomo zaidi status
 

Attachments

  • IMG-20241119-WA0050.jpg
    IMG-20241119-WA0050.jpg
    227 KB · Views: 14
Watu wanao nunua hisa ili wapate dividend wanapata faida ndogo sana.

Unaponunua hisa kuna makato ya Broker,DSE,CMSA etc na unapouza pia vile vile.Alafu unakuta gawio ni la 8.XX%

Ujanja ni kujua lini unanunua na kuuza hisa.
 
Back
Top Bottom