Fanya haya ukikutana na daktari

Fanya haya ukikutana na daktari

Ozzie

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2007
Posts
3,217
Reaction score
1,261
1. Usidanganye/

2. Mpe daktari sababu za kumtembelea. Kawaida sababu ni dalili, na si jina la ugonjwa udhaniao wakusumbua. Mfano kuna tofauti kubwa mtu akienda kwa daktari akasema ninajisikia viungo kuuma, mwili kuwa wa moto, kutapika na kukojoa sana; ukimfananisha na yule atakayesema dokta mimi nimekuja kwa sababu najisikia nina Malaria. Hizo dalili za "Malaria" zinaweza zikawa dalili za ugonjwa wowote wa maambukizi. Hivyo mtu wa kwanza kampa daktari nafasi ya kufikiria magonjwa yenye hizo dalili, wakati mtu wa pili anamzuia daktari kufikiria nje ya box. Mwache daktari atumie kichwa kujua dalili za ugonjwa wako zinahusiana na ugonjwa gani.

N. B: Kuna magonjwa sugu kama Kisukari, hypertension, HIV/AIDS n.k.ambayo huna budi kumwambia daktari pindi unapopata tiba.

3. Ukienda kwa daktari au maabara, usipende kumwambia nataka kupima Malaria au Amoeba au maswali kama hayo. Ukikutana na watumishi wasio waaminifu watakuchukua damu, mkojo na au choo kubwa na kuzunguka nayo kwenye maabara. Watapoteza muda huko na kurudi na majibu uliyokuwa ukitaka. Wengi wetu tunaridhika sana kuambiwa twaumwa kitu tunachofikiria. Utasikia mtu anasema, "unaona, mimi nilishasema; nikiwa na dalili xxx huwa ninakuwa nina ugonjwa yyy". Kumbe umeliwa, kipimo hujafanyiwa na dawa utanunua. Usijifanye chakula cha madaktari au watumishi wa afya fake. Waache watumie akili kujua uumwacho.

4. Usisahau kumwambia daktari dawa ulizotumia.

5. Usiache maswali au hofu yako.

6. Kama una vipimo ulifanya nyuma, labda X ray, ultrasound, vipimo vya damu, ecg n.k. Waweza ambatana navyo.

7. Usiogope kupishana na daktari.

8. Hakikisha unafuata tiba uliyoandikiwa.

9. Usihamehame toka daktari mmoja hadi mwingine, mpaka pale inapobidi. Chagua daktari mapema. Jengeni hali ya kuaminiana.

10. Uliza kazi za dawa upewazo, na hakikisha unatunza kumbukumbu.
 
1. Usidanganye

Excellent
 
Dr... Najisikia kuumwa maralia na hivyo nahitajia uniandikie mseto nikameze mbili kutwa Mara tatu.
 
Ushauri mzuri manake mimi huwa namwambia doctor nina dalili za uti.
 
Madaktari wana nyodo. Huwa hawapendi kuingiliwa... utaskia "unanifundisha kazi?" Kama una pesa ni bora uende private. Govt kuna ukakasi sana sote twajua hili. Hivyo kuna baadhi ya hoja hapo juu ni ngumu kutekelezeka ktk vituo vya afya au zahanati
 
Sikuhizi madaktari wamekuwa hovyo sana..juzi nimepatwa na jeraha nikaenda dispensary karibu na ninapoishi ili nichomwe sindano ya tetenasi badala yake nikachomwa na kile kifaa cha kutobolea kidole wakat wa kipimwa malaria..
Eti ndio tetenasi
 
Mi nashukuru nipo vizuri ktk kujielezea kwa doctor iila tatizo langu hua nahisi uvivu kwenda hospital na nikienda najihisi nazidiwa
 
Full kuwakomalia mm nikiwa naumwa nakuwa mkali sana na ujasili wa hali ya juu doctor akileta mapozi nampa makavu. Ngoja cku wanigonge nusu kaputi nikomeeee...
 
Niliwahi kwenda kwa Dr mmoja maeneo ya Mnazimmoja hapa Dar es Salaam,nikamweleza jinsi ninavyojiskia,hapo hapo,kaandika dawa na kuniambia nikanunue dirishani.Nikamwomba Dr sasa,mbona hata hatujadiliani walau kunieleza haya yanasababishwa na nini❔❔➖Daktari yule alibadilika ghafla Sana,akaanza kutukana ya kwamba namfundisha kazi.Mimi nikaondoka zangu taratibu.Bado tuna shida,wasomi wengi WA nchi hii,hawana elimu ya customer care kwa wateja wao.Ni matatizo
 
Umenena Mkuu,
 
ASANTE USHAURI WAKO NI MZURI SANA.

Sitahau kamwe kwenye maisha yangu pale Dr.mmoja wa gv hosp alipomwandikia mwanangu dawa ambazo alikatazwa asinywe kabisa zinamdhuru wazi wazi . Nikamwambia mapema/ kwa uwazi kabisa kuwa mwanangu dawa za aina fulani HARUHUSIWI KUTUMIA tena aliambiwa na Dr specialist wa MNH. Alichonijibu kuwa nisimfundishe kazi hiyo ndiyo dawa anayoona inamfaa kumtibu. Nikashtuka sana. Aliponiandikia zile dawa sikununua. Bahati mzuri nilienda wakati ndiyo anajiandaa kumaliza shifti yake. Alipoondoka na kuingia Dr mwingine nilienda kumwona Dr. Yule Dr nikamwelezea akanielewa vizuri, ila alisikitika sana tena akasema ulifanya la maana kutokununua na kumpa huyo mtoto lasivyo kungetokea tatizo kubwa la kiafya kwa mtoto. Akamwandikia matibabu mengine ,mtoto akapona vizuri. Na akasema ataongea na yule Dr 0 (nimemwita 0 ksb hafahamu madhara ya uzembe au ujinga wake ).Mpaka leo yule Dr NAMHESHIMU NA KUMSHUKURU SANA. KILA NIKITAKA KWENDA HOSP HIYO BASI LAZIMA NTAMTAFUTA KSB NDIYE NILIYE NA IMANI NAYE KWA MATIBABU YA MWANANGU.
DR mwanamke ndiye aliyemwandikia dawa za kumdhuru mwanangu na Dr mwanamke pia ndiye aliyemwepusha na kumwokoa mwanangu.
BAADHI YA MA DR TANZANIA NI MAJANGA USIPOKUWA MAKINI UNAWEZA KUPATA MADHARA KUTOKANA NA TIBA ZAO. ILA BAADHI YAO WANAUFAHAMU WA KUTOSHA KUHUSU UTAALAM WAO.
Customer care TZ kwa BAADHI YA MA DR hasa kwa gvment Hosp mhh!! Yataka MOYO .
 
Back
Top Bottom