Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,261
1. Usidanganye/
2. Mpe daktari sababu za kumtembelea. Kawaida sababu ni dalili, na si jina la ugonjwa udhaniao wakusumbua. Mfano kuna tofauti kubwa mtu akienda kwa daktari akasema ninajisikia viungo kuuma, mwili kuwa wa moto, kutapika na kukojoa sana; ukimfananisha na yule atakayesema dokta mimi nimekuja kwa sababu najisikia nina Malaria. Hizo dalili za "Malaria" zinaweza zikawa dalili za ugonjwa wowote wa maambukizi. Hivyo mtu wa kwanza kampa daktari nafasi ya kufikiria magonjwa yenye hizo dalili, wakati mtu wa pili anamzuia daktari kufikiria nje ya box. Mwache daktari atumie kichwa kujua dalili za ugonjwa wako zinahusiana na ugonjwa gani.
N. B: Kuna magonjwa sugu kama Kisukari, hypertension, HIV/AIDS n.k.ambayo huna budi kumwambia daktari pindi unapopata tiba.
3. Ukienda kwa daktari au maabara, usipende kumwambia nataka kupima Malaria au Amoeba au maswali kama hayo. Ukikutana na watumishi wasio waaminifu watakuchukua damu, mkojo na au choo kubwa na kuzunguka nayo kwenye maabara. Watapoteza muda huko na kurudi na majibu uliyokuwa ukitaka. Wengi wetu tunaridhika sana kuambiwa twaumwa kitu tunachofikiria. Utasikia mtu anasema, "unaona, mimi nilishasema; nikiwa na dalili xxx huwa ninakuwa nina ugonjwa yyy". Kumbe umeliwa, kipimo hujafanyiwa na dawa utanunua. Usijifanye chakula cha madaktari au watumishi wa afya fake. Waache watumie akili kujua uumwacho.
4. Usisahau kumwambia daktari dawa ulizotumia.
5. Usiache maswali au hofu yako.
6. Kama una vipimo ulifanya nyuma, labda X ray, ultrasound, vipimo vya damu, ecg n.k. Waweza ambatana navyo.
7. Usiogope kupishana na daktari.
8. Hakikisha unafuata tiba uliyoandikiwa.
9. Usihamehame toka daktari mmoja hadi mwingine, mpaka pale inapobidi. Chagua daktari mapema. Jengeni hali ya kuaminiana.
10. Uliza kazi za dawa upewazo, na hakikisha unatunza kumbukumbu.