osu2014
Member
- Mar 31, 2014
- 20
- 54
Wakuu,
Mtaalan kumekuwa na story nyingi sana za watu kutekwa.Wengine wakiwa marafiki wengine ndugu na sisi wengine kusikia kutoka kwa vyombo vya habari kwamba yule au huyu katekwa au hajulikani alipo.
Katika pita pita zangu za Maisha hapa duniani niliwahi kufundishwa kanuni nyingi za kujilinda na njia za kufanya unapogundua upo hatarini. Leo nitaelezea chache labda kwa uzi huu naweza kuwa nimemsaidia mtu kwa njia moja au nyingine.
Njia ya Kwanza kabisa.(Situational Awareness)
Kama unajua wewe una adui(Iwe serikali au Mtu binafsi wakati wowote ukiingia au ukiwa sehemu kuwa na uelewa wa mazingira yaliyokuzunguka. Kama ni mgahawani angalia watu wote uliowakuta na hakikisha hata kukaa kwako uchague kiti ambacho kitatizama mlangoni ili uone nani anaingia.
Kama uko kwenye gari hakikisha kila baada ya sekunde 10 unaangalia Side Mirror zako kujua kuna gari gani nyuma yako au pembeni yako au kama kuna gari au bodaboda imekufuatilia muda mrefu. Ukiona gari imekuwa nyuma yako muda mrefu jaribi kuongeza mwendo uone kama naye ataongeza. Jaribu pia kupunguza mwendo ili aovertake hii yote ni kuhakikisha uko salama.
Ya Pili(Baseline Observation)
Hii ni kuangalia uhusiano wa vitu na matukio. Mfano tumezoea ukienda beach kuna aina ya Mavazi utaona watu wamevaa mfano Bikini, Bukta, wamevaa either kofia za Jua, au miwani. Hatutegemei kuona beach mtu amevaa nguo au viatu vya kijeshi(Tactical gears)Yaan hapa unatakiwa unotice vitu ambavyo vipo out of place.
Mfano unarudi nyumbani kila siku lazima ukute mlinzi getini siku hiyo hakuna mlinzi lazima ushtuke(Kumbuka story za Lissu siku amepigwa risasi)Au unatembea barabarani unaona barabara siku zote inakuwa busy lakini gafla siku hiyo uko peke yako tu.
Rejea mauaji ya Sheikh Aboud Rogo huko Mombasa, Ambapo barabara nzima walikuwa wako wanaendesha ila wanaona hakuna gari lolote zaidi yao hadi pale gari lao lilipomiminiwa risasi 15 na kumuua hapo hapo na mkewe akinusurika.
Tatu acha ratiba kuwa na ratiba zinazotabirika(Pattern of Life)
Hii inajumulisha kuwa na tabia ya kwenda kazini muda fulani kila siku, Kutoka kazini muda fulani kila siku, Kupita njia moja kwenda na kurudi kutoka kazini na Kadhalika. Ukiwa unajua uko hatarini jitahisi sana usiwe na ratiba inayoeleweka. Utanishukuru siku moja.
Ya Mwisho kwa leo ni Escape Plan
Siku zozote ukienda sehemu lazima ukague au just google maeneo ya kutorokea kama ikitokea shida. Kama umeitwa hotel flani muda flani jitahidi uwahi ukague eneo kabla ya unakuja kukutana nao. Ukienda hotelini kagua milango ya dharura, Angalia dirisha la chumba chako, Angalia chumba ambacho ikitokea lolote utaweza kuwa na plan b…
Mnisamehe tu nimeandika haraka haraka.