Fanya haya utakapo kuwa umepotea njia msituni

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Hatua za kuchukua unapogundua kuwa umepotea njia msituni fuata haya!

Hatua ya Kwanza.

angalia kwanza ni muda gani umepita au ni dakika ngapi zimepita tangu umegundua kuwa upo kwenye njia isiyo sahihi.

Hatua ya pili.

Kisha kumbuka njia au uelekeo uliopita hadi kukufikisha hapo ulipo jihisi kuwa umepotea.

Hatua ya tatu.

Rudi nyuma kuifuatisha hiyo njia moja kwa moja kwa kuzingatia muda ule ule ulio tumia kutoka sehemu sahihi hadi sehemu uliopotea.

Hatua ya nne.

Kisha ukifika eneo ambalo umejihisi hujapotea kisha tafuta njia sahihi kutokea hapo na uifuate kama umepotea tena hakikisha unarudia hivyo mara kwa mara itakusaidia kupata muelekeo sahihi.

Angalizo !

Iwapo utagundua kuwa umepotea msituni usianze kutafuta njia sahihi bila kurudi nyuma mpaka kwenye sehemu ambayo ulijihisi ujapotea kwani kwa kufanya hivyo itapelekea upotee zaidi msituni unashauriwa kurudi nyuma kwanza hadi kwenye eneo unalojihisi hujapotea hapo ndipo upatumie kutafuta uelekeo sahihi.

Je, umewai kupotea njia porini (msituni) ukapata shida sana kutafuta uelekeo sahihi wa njia ?
 
Kino Boys hawawezi kuelewa hizi mambo.

NYONGEZA : Ukikutana na Simba huko msituni, vua nguo zote huku ukimkazia macho. Kisha kwa kujiamini anza kumsogelea taratibu. Simba atatimua mbio kwasababu atakua anajiuliza mnyama gani huyu mwenye mkia mbele.

Angalizo, hii njia haifanyi kazi kwa wanawake.
 
Dah! Hii kitu isikie kwa mtu kama story aise! Sijui hata akili inakuwaje. Iliwahi nitokea, wenzangu wakaniacha nyuma. Mi najua nikikatiza uelekeo wa njia ntawapata. Acha weee! Nafika sehemu kwa mbele, naona maji tu. Kuogelea, sijawahi. Kurudi nyuma natokezea kwingine. Kama baada ya masaa 7, nilibahatika kusikia muungulumo wa gari. Nikaelekea nilipousikia. Kufika, sijui nielekee wapi. Nilikaa hapo hapo mpaka jioni ndo likapita gari jingine, nilijieleza nikaeleweka, na kusaidiwa. Mpaka wa leo hili jambo linanikaa akilini kama movie. Unakatiza sehemu unakutana na lijoka hujawahi kuona maishani. Mengine yanadhalau balaa.
 
Kuzubaa tu unapoteaje porini
 
Hatua za kuchukua unapogundua kuwa umepotea njia msituni fuata haya!

Hatua ya Kwanza.

angalia kwanza ni muda gani umepita au ni dakika ngapi zimepita tangu umegundua kuwa upo kwenye njia isiyo sahihi.

Hatua ya pili.

Kisha kumbuka njia au uelekeo uliopita hadi kukufikisha hapo ulipo jihisi kuwa umepotea.

Hatua ya tatu.

Rudi nyuma kuifuatisha hiyo njia moja kwa moja kwa kuzingatia muda ule ule ulio tumia kutoka sehemu sahihi hadi sehemu uliopotea.

Hatua ya nne.

Kisha ukifika eneo ambalo umejihisi hujapotea kisha tafuta njia sahihi kutokea hapo na uifuate kama umepotea tena hakikisha unarudia hivyo mara kwa mara itakusaidia kupata muelekeo sahihi.

Angalizo !

Iwapo utagundua kuwa umepotea msituni usianze kutafuta njia sahihi bila kurudi nyuma mpaka kwenye sehemu ambayo ulijihisi ujapotea kwani kwa kufanya hivyo itapelekea upotee zaidi msituni unashauriwa kurudi nyuma kwanza hadi kwenye eneo unalojihisi hujapotea hapo ndipo upatumie kutafuta uelekeo sahihi.

Je, umewai kupotea njia porini (msituni) ukapata shida sana kutafuta uelekeo sahihi wa njia ?
Lishe ya ubongo
 
Pole sana unapogundua kuwa umepotea jaribu kushusha presha alafu vaa ujasiri na ufuate maelekezo yangu hapo juu itakusaidia hata kurudi eneo ambalo mlikuwa na marafiki zako ukapata msaada wa haraka lakini kuzunguka zunguka hovyo msituni kunaweza kukupelekea upotee zaidi na hata kukutana na wanyama wakali
 
NITAKUJA NA KISA CHANGU NILIPOTEA MSITU WA LIKUYU...NAMTUMBO....SELOUS...NIKIWA NA MZEE SAIDI GOYAGOYA
 
Je, umewai kupotea njia porini (msituni) ukapata shida sana kutafuta uelekeo sahihi wa njia ?
Ndio na nilitukanwa sana na yule mtu siku hio ilikua usiku ila nilitumia akili nikafanikiwa kufika ninapoenda na nikafika salama, karibu machakani nilirudi nyuma kule nilipokua naenda ndio nilikua napotea zaidi nikarudi nyuma kuanza upya ndio nikaiona njia ya ninapoelekea maporini kupotea sio ajabu
 
Kuna watu watapuuzia ulicho andika lakini kwa tuliowai kupoteza porini tunajua shughuli yake..Bora mpotee mkiwa wawili mnaweza ongeza nguvu ya akili na kushusha presha kuliko ukiwa peke yako... Porini kunatisha..
Alafu watu waelewe tofauti ya porini,msituni na vichani
 
Nilishawahi kwenda kwenye msitu mmoja njia pekee ya kutokupotea ilibidi kila tupopita tunaweka alama kwenye mti kwa kukata panga vinginevyo ukitumia hiyo njia yako uliyoisema hutoboi maana miti ni mirefu na mazingira yote ya ndani yanafanana
 
Ndo nimekwambia kuna kitu mpaka sasa sijaelewa, kuzubaa huko kunaanzaje! Ni sawa na uulize mtu anaibiwaje!
Umeshawahi kusikia huu uyoga unaitwa magic mushroom, ukiukanyaga unatoa vumbivumbi halafu ulihemea hili vumbi unashangaa unaanza kuwa zoba bila kujielewa, na ndio watu wengi wanapotelea maporini unajikuta unazunguka humohumo bila kujua njia ya kutokea

1738187918455.png
 
Nilishawahi kwenda kwenye msitu mmoja njia pekee ya kutokupotea ilibidi kila tupopita tunaweka alama kwenye mti kwa kukata panga vinginevyo ukitumia hiyo njia yako uliyoisema hutoboi maana miti ni mirefu na mazingira yote ya ndani yanafanana
mbwa muhimu kutembea nayo au kufuga hutakuja potea....hukojoa kila baada ya hatua 10 mkiaza tu kupotea maeneo inayoyajua
 
Upo sahihi ,, mwaka 2017 tulienda iringa ,,kijijini tulishukia eneo moja linaitwa madisi tukarnda ndani ndani huko,, tulienda kule kuangalia shamba la miti ya mbao la jamaa yetu mmoja

Sasa kule usafiri ni pikipiki tu aina ya fekon ( mchina ) tulikuwa watu watatu na dereva tunakuwa 4 ,,hivyo kutokana na hali ya miinuko (milima ) iliyoko kule tulishindwa kupanda wote ,,, wazo likatolewa wawili plus dereva watangulie afu mimi niwe nafuata nyuma lengo likiwa dereva akishawafikisha shambani wale wawilj arudi kwangu kuja kunichukua ila ili isirudi tena kwa umbali mrefu na kutumia mafuta mengi nikaombwa niwe nasogea mdogo mdogo huku nikiwa nimeleekezwa njia ya kufuata..

Sikuwa na wasiwasi kule wanyama wakali kama nyoka na simba hawapo ,, wezi hawapo licha ya kuwa na misitu ya kutosha ,, sasa basi katika kuifuata njia ile kwa muda kama wa saa moja hivi nikakutana na njia panda ,, dereva alisahau kunielekeza hapa nichukue njia ya upande upi ,,, hapa nilikuta njia mbili ya mkono wa kushoto na mkono wa kulia ,, ya mkono wa kushoto inaonekana ni njia inayotumika sanaa ila ya kulia inamajani mengi nikaona hii itakiwa siyo mbona watu hawapiti basi mimi nikafuata ya mkono wakushoto ambayo nimepotea ,, aisee nilitembea umbali mrefu sana nilitumia muda wa masaa mawili network hamna masna ni misitu ya miti ya mbao tu imetawala na kilichopelekea nitembee umbali wote ule mwanzo nilikuta na watu wawili wakitokea njia ile japo walionesha kunishangaa lakini sikujali nikafika mahala njia ikapotelea kwenye vichaka vya miti jambo lilopelekea nisite kuendelea kwenda mbele

Akili ikarudi kuwa hapa nimepotea ikanibidi nianze kurudi nyuma baada ya kutembea kwa muda wa nusu saa nakutana na pikipiki ikiwa na yulee dereva aliponiona hakuamini anadai amenitafuta mnoo kaenda na kurudi mpaka kule tulipofikia mara 4 ,, kasha toa raarifa kwa mwenyekiti wa kising'a kuwa nimepotea kuja na hii njia huku alikuwa anajaribu kwa mara 2 ...

Nafika kijijini nakuta watu wamejaa habari zilizotawala ni kuhusu mimi kupotea ,, jamaa mmoja akaniambia unabahati sana giza lingekukuta huko huenda ungechukuliwa msukule maana ile njia inaenda kwenye muiniko ambao watu huenda kufanyia ibada ( tambiko ) na mambo yao mengine ..
 
Pole sana unapogundua kuwa umepotea jaribu kushusha presha alafu vaa ujasiri na ufuate maelekezo yangu hapo juu itakusaidia hata kurudi eneo ambalo mlikuwa na marafiki zako ukapata msaada wa haraka lakini kuzunguka zunguka hovyo msituni kunaweza kukupelekea upotee zaidi na hata kukutana na wanyama wakali
Njia nyingine ukipotea porini badilisha nguo uliyovaa ndani weka nje na nje weka ndani utakuja nishukuru
 
Tuliwahi kuachwa msituni tujiendee wenyewe na kina bibi fulani waliokuwa wanafahamu miiko ya kuenenda porini. Wanasema ukipotea msituni piga kimya usiwaambie wenzako kuwa umepotea, ukiwaambia tu mnapotea wote na hakutakuwa mtu wa kuwaongoza njia sahihi. Wale mabibi walijitenga na sisi kwa kutuona ni waropokaji wa mambo tunayoyaona msituni. Waliona tutapotea wote na kukosa tulichoenda kukitafuta porini. Tulienda kuchuma na kuokota matunda pori kwa ajili ya lishe. Kule hata ukiona wayo wa simba (fingaer print) hutakiwi kutamka simba, unatamka ng'ombe wa porini au mfalme wa pori. Wanaamini ukitamka simba atatokea na kuleta shida. Porini/msituni unaweza kupoteza dira usijue wapi ni kaskazini, kusini, mashariki na magharibi, hutajua jua linatoka wapi na kuelekea wapi kwa usahihi, mambo huvurugika unaweza kuona jua linatoka kaskazini kwenda kusini au magharibr kwenda mashariki au kusini kwenda kaskazini ukaishia kwenda uelekeo usio sahihi na kuzidi kupotea zaidi. Ni hatari mnaweza kukesha porini msijue mpo wapi
 
Back
Top Bottom