Fanya hivi kubana matumizi

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
Hali ya maisha sasa hivi imekuwa ni tofauti, makampuni yanabana matumizi hivyo nasisi lazima tubane matumizi. Hizi ni mbinu unazoweza kuzitumia kubana matumizi
1. ukifanya maamuzi ya kuishi tafuta mahala ambapo ni karibu na ofisini kwako
2. ukiwa ndani ya nyumba zima taa katika vyumba ambavyo havitumiki
3. Kama una mahusiano mazuri na wafanyakazi na mnakaa karibu wekeni mpango wa kutumia gari moja ili mchangie mafuta
4. epuka kula nje ya nyumba ukiweza pika mwenyewe nyumbani
5. chagua harusi za kuchangia usichangie kila harusi
6. badala ya kulipia channel 150 kwenye king'amuzi lipia channels unazoangalia tu
7. badala ya kulipia gym jiunge na jogging clubs na fanya mazoezi mwenyewe (programs zipo kwenye internet)
8. ukitoka out na mtu mwambie kuwa kila mtu atajilipia bili yake
9. Ukienda kazini toka na baadhi ya vyakula ambavyo mjini ni gharama au havipatikani kama matunda
10 mtu akikuomba hela ghafla pima uzito wa maombi vinginevyo mwambie haiko kwenye bajeti mpaka utakapopanga bajeti nyingine.
11. ukinunua taa nyumbani nunua zinazotumia umeme kidogo
12. usipende kutembea usiku lolote linaweza likatokea likakugharimu pesa
13. usipende kuazima kitu cha mtu kikipata tatizo huna namna zaidi ya kulipa wakati ambao hauna hiyo bajeti 1
4. Nguo unazoweza kufua nyumbani usipeleke dry cleaner

sent from posta
 
Usiandike visivyowezekana

.... you can't convince, then confuse....
 
Sawa mkuu pambana tu na hali yako
 
Sioni kinachonihusu hapo.. gari,dry cleaner,gym ,chanel 150

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini ubane matumizi mkuu? Sera ya kubana matumizi iwe ni kwa mtu au nchi tafsiri yake ni moja tu mtu huyo au nchi iyo ilikuwa limbukeni ya matumizi na kwamba ilielekeza pesa zake kwny mambo ya kiuasherati.

Being frugal in busines n life z good lakini isifikie hatua ya 'kujinyima'. Kama unapenda kula vizuri,kutembelea mkoko mzuri,kuvaa vizuri au spending on lavish vacations hizo sio anasa ni kujipenda na kuthamini maisha

Unachotakiwa kufanya ni kuumiza kichwa tu how u will maintain yo lifestyle, n this means uongeze creativenes by awakening yo geniusness kubuni other sourcs v income that will keep bringing money in yo pocket.

One v my busines mentors hupenda kusema 'mtumiaji ni mtu anaejua kutafuta lkn mbanaji ni lofa wa ugunduzi'

Mkuu life z too short to deal with cheap drinks,cheap food n being average.

#G.T.O
 
Mkuu, yaani katika list yako, hakuna hata moja ambalo linamgusa mtu mwenye maisha ya chini..

Anyway, wafanyakazi na wenye magari wamekusikia
Kama ukitoka nyumbani kwako kwenda kituo kikuu cha bus unatumia bodaboda au noah, amka asubuhi sana kisha tembea kwa miguu kufidia muda na gharama za nauli

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
 
Hilo ndiyo jambo napambana nalo kilasiku, ni vipi nitakavyo maintain my lifestyle huku mambo mengine yakiendelea kama ninavyo plan yawe

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
 
Jaribu kununua vitu vya ndani kwa bei ya jumla

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Poa

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Kutokula kwa mama ntilie, kuish karibu na ofsn, usikopeshe ovyo, kuzima taa nk nadhani vingi vinawagusa hata watu wa hali ya chini asante mkuu

Sent from my itel it1409 using JamiiForums mobile app
 
Vimenigusa vyote nashukuru sana nitavifanyia kazi, maana naishi mbali na ofsin almost 30km kwenda then 30km kurudi. Nimemshawish wife tukapange karibu na office hataki,
kwa siku natumia mafuta ya 15000 pia njia ni mbovu hivyo service za Mara kwa Mara zinanihusu .

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni tajiri ila hujaamua kupanga mikakati vizuri

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…