Fanya hivi kuepuka kukosa mawasiliano utakapofungiwa na TCRA kama hujasajili kwa alama za vidole

Fanya hivi kuepuka kukosa mawasiliano utakapofungiwa na TCRA kama hujasajili kwa alama za vidole

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Muda wa kutumia simu kadi ambazo hazijasajiliwa unafika ukingoni January 20 huku kukiwa na siku mbili tu mbele.

Watanzania lukuki bado hawajakamilisha zoezi hili muhimu huku sababu kubwa ikitajwa ni NIDA kuwa na mwendo wa kinyonga, pamoja na hayo TCRA wametoa msisitizo kuwa hawataongeza muda wa usajili.

Unachopaswa kufanya:
Kama itafika January 20 na hujakamilisha zoezi la usajili unapaswa kuchukua.

Hatua hizi huku ukiendelea kuhangaikia lakini yako kufunguliwa mpaka hapo utakapokamilisha usajili.

1. Jiunganishe na huduma zinazowezesha mawasiliano mbadala, mfano WIFI ambayo haihitaji simu kadi ili kuweza kufanya kazi, hapo utaweza kupiga voice call Whatsaap, kuchati mtandao ya kijamii, kuwasiliana kwa barua pepe n.k

2. Azima simu kadi iliyosajiliwa. Unapaswa kumtafuta mtu anayekuamini na ukiwa alisajili lakini zaidi ya mbili muombe kuazimieshe

3. Tumia mawasiliano mbadala, kama vile kutumia barua kuwasiliana na njia nyinginezo.

4. Tumia PayPal, bank, webmoney, nk kutuma na kupokea fedha. Simu iliyounganishwa na WIFI au mifumo mingine inayoweza kukuunganisha na internet hata simu ya rafiki yako inaweza kukusaidia katika hili.

Vilevile unaweza kutuma na kupokea fedha kupitia kwa mawakala wa mitandao ya simu mtaani kwako, yani anatuma moja kwa moja kwa wakala.

Usikubali biashara au shughuli zako zikwame kisa hujakamilisha usajili baada ya January 20. Wakati ukishughulikia mchakato njia hizo ni mwarobaini wako

FB_IMG_1579332578269.jpg
 
Kuna mdeni wangu ananisumbua sana kwenye sm sasa nasikia bado ajakamilisha usajili yani nazidi muombea njaa usajili usikamilike ili aache nisumbua kabisa
 
Haijalishi kabla ya hizi kamupuni za simu tulikuwa hatuishi vizuri hatuwasiliani na ndugu zetu maana hizi teknoligia zilikuja kwetu ndugu zetu walipozipokea wakawa malimbukeni Bora wafunge tu hakuna maana wengi hawajui faida ya mawasiliano
 
hivi kama unadaidawa na hawa jamaa watakufanyaje wakati line isharudi kwao.M PAWA.NIWEZESHE.TALA.BRANCH.Na wengine wanakopesha watu kimtandao.au ndio wamesamehewa deni bila wao kujua mungu ni mwema sana
 
Kuna mdeni wangu ananisumbua sana kwenye sm sasa nasikia bado ajakamilisha usajili yani nazidi muombea njaa usajili usikamilike ili aache nisumbua kabisa
Duh 😎😎, ni mimi ujue, naenda kusajilia kitambulisho cha mtu leo.
 
Back
Top Bottom