the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Wakuu mpo salama?
Naimani kuwa Kila mfanyabishara ama mtoa huduma anahitaji kuwashawishi wateja wake wanunue bidhaa ama huduma anayoitoa jambo ambalo si rahisi pia kama hutojipanga vyema
Kila mteja kabla ya kunua bidhaa kuna vitu ambavyo vinaweza kumfanya asinunue hiyo bidhaa anaweza kuwa navyo vyote au kimojawapo kati ya hivi vifuatavyo na wewe kama mfanyabiashara ama mtoa huduma unapaswa kuhakikisha licha ya vikwazo hivyo kutoka kwa mteja basi uweze kumfanya abadili maamuzi na kuinunua hiyo bidhaa ama huduma.
Kutokuwa na pesa.
Mteja anaweza kusema kuwa hana pesa ya kununua bidhaa yako ama huduma unayoitoa kwa kuhofia kuwa pengine unaitoa kwa kiwango kikubwa cha fedha na hivyo kumfanya asiendelee na manunuzi hayo. Jukumu lako kama mfanya biashara ama mtoa huduma ni kuhakikisha unamfanya mteja wako aone kuwa anaweza kumudu gharama za bidhaa ama huduma uitoayo na kuweka mikakati mizuri kuhakikisha kwa kiwango kikubwa wateja wanaweza kujiona kuwa wanamudu huduma hiyo. Mfano unaweza kuzifungasha bidhaa zako katika viwango tofauti tofauti mfano ½ kg, 1kg, 5k nk kulingana na huduma ama bidha uliyo nayo ili kuhakikisha kila mtu anaweza kumudu na na kuondokana na ile hofu ya kusema kuwa hana pesa ya kumudu.
Kutokuona kama ana uhitaji.
Mteja anaweza kuona kuwa hana uhitaji na hiyo bidhaa yako au huduma unayotaka kumpatia kwa wakati huo, hivyo una wajibu wa kumshawishi kwa kumpa elimu ya kina kuhusu bidhaa yako ama huduma unayoitoa ili aone uhitaji wa kuwa na bidhaa hiyo au kupokea huduma unayoitoa. Mfano kama unauza asali unaweza kumuelezea faida ya kuwa na hiyo bidhaa, unaweza kumueleza kuwa asali inaweza kumpatia faida gani mathalani kwa upande wa afya hii inaweza kumfanya mteja aone kweli anahitaji bidhaa hiyo na kuichukua.
Kutokuwa na Imani.
Hapa mteja anakuwa hana Imani na bidhaa yako ama huduma unayoitoa hivyo kuleta ugumu kwake kununua bidhaa hiyo kutoka kwako, na hii kwa wakati mwingine inaweza kuwa imesababishwa na kadhia aliyokutana nayo hapo kabla kutoka kwa muuzaji au mtoa huduma mwingine kabla yako. Mteja wa aina hii anapaswa kupewa ushuhuda au Ushahidi wa kutosha kumfanya aweze kuiamini bidhaa au huduma yako. Mfano unaweza kumkututanisha na wateja wako wa siku zote au wa mara kwa mara, ama kumuonesha matokeo yaliyotokana na watu kutumia bidhaa au huduma yako ili kuirejesha ama kuikuza Imani yake. Na kwa kuwa hivi sasa kuna mitandao ya kijamii unaweza kuitumia hiyo kujenga jina lako na kuongeza Imani yako kwa watu.
Kutokuwa na matamanio/hamu na bidhaa hiyo.
Mteja anaweza kutokuwa na hamu ama matamanio na bidhaa hiyo ambapo hapa unatakiwa kumfanya mteja kuwa na hamu na bidhaa ama huduma hiyo. Mfano unaweza kumuelezea mchakato wa utengezaji wa bidhaa hiyo au utoaji wa huduma hiyo unavyotofautiana na huduma nyingine alizozizoea ili kumfanya mteja wako kuona kitu cha ziada kutoka kwenye biashara yako ama huduma unayoitoa na hivyo kumfanya awe na hamu ya kujaribu bidhaa ama huduma hiyo ili aweze kuona utofauti.
Kutokuwa na haraka na hiyo bidhaa.
Mteja wakati wingine anaweza kuona kuwa hana haraka sana na hiyo bidhaa, hivyo ni wajibu wako tena kama muuzaji ama mtoa huduma kumfanya mteja wako aone kuwa anahitaji bidhaa ama huduma hiyo kwa haraka. Muuzaji ama mtoa huduma unaweza kumtengenezea mteja Fear of missing out kwa kutumia njia mbali mbali mfano pata punguzo la bei msimu huu ama wiki hii, au nunua moja upate mbili ndani ya wiki hii nk, ili ashawishike kuipata bidhaa hiyo kwa haraka na asije kupitwa na ofa hiyo.