Fanya yafuatayo ili uweze kufanikiwa kwenye biashara ya bucha

Fanya yafuatayo ili uweze kufanikiwa kwenye biashara ya bucha

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
  • Uanzishapo biashara ya bucha, hakikisha pia una kijiwe cha nyama choma.​
  • Hii itakusaidia nyama kutokubaki, na kufanya fedha yako kuwa kwenye mzunguko.​
  • Hakikisha pia una wateja wako angalau kumi wa kudumu, iwe mama ntilie au wachoma mishikaki n.k​
  • Malengo kwa siku, angalau uuze kilo 50 na hakuna haja ya kuchukua/kununua kilo nyingi kwa siku (unaweza kununua kila 70 kwa siku).​
  • Na faida kwa kila kilo ni shilingi 1000; kwa hiyo kama utafanikiwa kwa kila mwezi, utakuwa unapata milioni 1.5, ukitoa gharama za uendeshaji unaweza kubaki na faida yako ya laki 8.​
  • Ukiwa nazo tano, utakuwa unatengeneza milioni 4​
  • Aya ingia mzigoni.​
 
Wamekusikia,shukrani
Sawa mkuu, changamoto niliyoiona kwa wenye mabucha wengi, wao sio sehemu ya walaji wa bidhaa yao; hii inapelekea nyama kubaki na kuona hiyo biashara hailipi.
Hii biashara inalipa na wapo wanaochinja zaidi ya ng'ombe watano kwa siku; muhimu ni kuwa na mkakati thabiti ya walaji wako.​
 
Biashara mtandao.
Haya haya haya mkujeeeeee
Unatakiwa uchukue ili wazo ufanyie utekelezaji; hata yale majengo marefu ya Dubai yalianzia kichwani
 
Unatakiwa uchukue ili wazo ufanyie utekelezaji; hata yale majengo marefu ya Dubai yalianzia kichwani
Naheshimu mawazo yako mkuu.
Nadhani wenye akili na mtaji watayafanyia kazi na kuyaingiza katika utekelezaji.
 
Fungua bucha, pia uanzishe kijiwe cha nyama choma; kuna siku nilikuwa maeneo ya manyara, watu wanakula nyama; acha kula tembele utauchosha mwili 😀
Nimeipenda idea.. Asante kwa madini,tutayafanyia kazi,
 
Naheshimu mawazo yako mkuu.
Nadhani wenye akili na mtaji watayafanyia kazi na kuyaingiza katika utekelezaji.
Kuna siku nilikuwa maeneo ya Iringa; bucha ya kitimoto na kwa pembeni wanakukaangia kama utapenda, kwa kifupi wanunuzi walikuwa wakija wanakuta 'stock' imeisha.
Nilitamani kama ingekuwa makazi yangu huko, ningekusanya hizo chenji zao.​
 
Riziki hupatikana pale ilipoandikiwa.
Usikute ungeenda huko mambo yangekuwa holaaaa.
 
Asante ,mimi nipo kwenye mchakato ,nilianzisha ndogo kwanza ya kufanyia visibility study lakini nilikosea chagua eneo bucha ikafa .

natafuta location nzuri maeneo ya hapa hapa dar es salaam.

Mwenye connection ya location nzuri
 
Tafuta penye makazi wengi wa watu
 
Back
Top Bottom