kalisheshe
JF-Expert Member
- Mar 19, 2020
- 2,064
- 4,056
Siasa ni maisha, siasa ni kila kitu katika taifa, ikiharibika siasa nyanja zote zimeharibikiwa ( elimu, uchumi, utamaduni na jamii). Hivyo basi hili ni jibu kwa wote wanaodhani siasa haihusiani na maisha Yao.
Fanya yafuatayo kama una ndoto ya kuwa mwanasiasa mzuri.
1. Kamilisha elimu yako (degree, diploma au cheti) kwa kusoma kozi za:- Sheria, uchumi, public administration na elimu. Hii itakusaidia kujua mambo mengi kuhusu uongozi na utawala.
2. Onekana ukijishughulisha na matatizo ya jamii
Jenga tabia ya kuonekana kwenye jamii ukisaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii, inaweza kuwa kwa kuzitatua au kuziripoti sehemu husika.
3. Tengeneza mahusiano mazuri na watu
Jitahidi kutengeneza mahusiano mazuri na kila mtu kwenye jamii yako, haijarishi Yuko upande wako au hakuungi mkono.
4. Fuatilia taarifa zote zinazojiri kwenye eneo lako, nchini au duniani
Hii itapanua uelewa wako kuhusu jamii unayoishi nayo, uongozi na uchumi.
5. Vaa vazi gumu (ngozi ngumu /roho ngumu)
Tegemea kuangushwa kwa kila namna na watu uliotegemea wakushike/ wakuunge mkono. Hivyo basi ili uishi vizuri jitengenezee roho ngumu ili usiishie kukata tamaa mapema.
6. Jijenge kiuchumi
Siasa za Africa zinahitaji pesa na ili ufanikishe rushwa haiepukiki kutoka kwa unaowaomba ridhaa, jiandae kwa hilo.
7. Kuwa karibu sana na Muumba
Sikufichi, kwenye siasa Kuna ushirikina wa kila namna. Kuna watu wametoa makafara mazito ili wapate nafasi. Kwa hiyo kama una nia ya dhati ya kupambana jiweke karibu mno na Muumba kwa kuziacha dhambi zote, kinyume chake ingia huko walikoingia wanasiasa wengi ili upate nguvu ya kupambana.
Tofauti na hivyo achana na siasa hutaweza.
Chukua hizo chache nitaendelea Tena.