SoC01 Fanya yafuatayo kwa mwanao kukabiliana na ukosefu wa ajira

SoC01 Fanya yafuatayo kwa mwanao kukabiliana na ukosefu wa ajira

Stories of Change - 2021 Competition

cilla

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
372
Reaction score
299
Mambo yamebadilika.dunia ya sasa inakabiliwa na tatizo la ajira kwa vijana na sisi kama walezi au wazazi tunapaswa kuwa na mitazamo tofauti kwa watoto wetu juu ya ajira.

Yafuatayo tunapaswa kufanya kwa kipindi hiki ili kuwajenga watoto wetu kuepuka janga la wasiokuwa na ajira baadaye:

(1) Tutambue vipaji na vipawa vya watoto mapema na kuviendeleza kwa bidii kama tunavyofanya kwa upande wa shule.Usiogope kugharimika kumuendeleza mwanao kwa kumpatia mwalimu au vifaa kwaajili ya kuendeleza kipaji chake .Huu si wakati wa kuhimiza mtoto kupata “A” tu jaribu kumuimiza kufanya ambacho ni kipaji chake kwa uzito .Kile anachokipenda au kile ambacho ndio kipaji chake kilee na kukikuza kwa kutafuta sehemu au mtu atakaye mnoa zaidi.

(2) Wafundishe wanao kile ulicho nacho.Ikiwa wewe ni mfanya biashara anza kumzoeza mwanao kusimamia na kuijua biashara zako.Ikiwezekana anza kuwaunganisha na wateja wako ili wateja waanze kumjua na kumzoea na mtoto wako aanze kuelewa yupi ni mteja muhimu na namna ambavyo unazungumza nao kama wateja.Taratibu mwanao ataanza kujua lugha ya kibiashara na kanuni zake.

(3) Ikiwa wewe ni fundi ,taratibu anza kwenda na mwanao katika kazi zako na kumzoeza kuzijua na kuzithamini.Usiache kumueleza umuhimu wa hiyo kazi na uzuri wake na kama haina manufaa kutokana na changamoto mbalimbali basi mueleze namna kazi hiyo ilivyo nzuri na kinachokukwamisha .

(4) Wakati wa likizo jaribu kumshikiza mwanao katika maeneo mbalimbali yatakayo msaidia kuwa na ujuzi na maarifa mbalimbali.Usikomae na tuition tu ikiwa maendeleo ya mwanao sio mabaya.Unaweza kumpeleka kujifunza kuogelea,kutumia kompyuta ,kuendesha gari,stationary,kupiga vyombo vya mziki,kuimba nk.

(5) Pendelea kwenda na mwanao maeneo mbali mbali unayopenda kwenda kama vile benki, kazini kwako, sehemu za kula na katika matembezi mbalimbali kwa sababu hii humjengea mtoto awereness na udadisi pamoja na kumjengea job career.

(6) Mwisho mjengee mtoto kujiamini kwa kumshirikisha mambo mbali mbali nyumbani na pia kumpa nafasi ya kufanya majukumu mbali mbali kama kuamua mle nini kwa siku hiyo,kuomba nk.

Usisahau mama wa elimu zote ni mazoezi (practice).
 
Upvote 3
Back
Top Bottom