Fao la Kujitoa NSSF

Fao la Kujitoa NSSF

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Wadau wa JF nisaidieni kwa haya:
  • Je NSSF bado wanatoa fao la kujitoa kwa watu walioacha au kufukuzwa kazi?
  • Je wanalipa pamoja na riba?riba kama ipo inakokotolewaje>
  • Je naweza fungua madai ofisi yoyote ya NSSF au Lazima niende pale niliposajiliwa mwanzo?
  • Je nikishajitoa ndio akaunti yangu imefungwa au naweza endelea kuitumia iwapo ninataka kuendelea kuitumia?
  • Je utaratibu mzima unachukua muda gani mpaka upewe pesa yako?
  • Je fomu zao zinapatikana wapi katika tovuti yao?au lazima niende kwenye ofisi zao?
Natanguliza shukrani zangu za dhati
 
Wadau wa JF nisaidieni kwa haya:
  • Je NSSF bado wanatoa fao la kujitoa kwa watu walioacha au kufukuzwa kazi?
  • Je wanalipa pamoja na riba?riba kama ipo inakokotolewaje>
  • Je naweza fungua madai ofisi yoyote ya NSSF au Lazima niende pale niliposajiliwa mwanzo?
  • Je nikishajitoa ndio akaunti yangu imefungwa au naweza endelea kuitumia iwapo ninataka kuendelea kuitumia?
  • Je utaratibu mzima unachukua muda gani mpaka upewe pesa yako?
  • Je fomu zao zinapatikana wapi katika tovuti yao?au lazima niende kwenye ofisi zao?
Natanguliza shukrani zangu za dhati
Kwa upande wa wafanyakazi wa serikali sijui ila tuliofanya kazi sekta binafsi ukiachishwa kazi inatakiwa ukae miezi 6 tangu uachishwe, baada ya miezi 6 inatakiwa uende kwenye lile tawi ulilofungulia/changia. Unatakiwa kwenda na barua yako ya employment termination au redundancy, utapewa form fulani upeleleke kwa muajiri wako ili kukujazia hela yako yote tangia uingie akionesha cheque namba/pay slip, baadae utairudisha nssf kwa ukaguzi zaidi. Baada ya kuhakikisha kuwa madai/hela yako imelipwa yote utapewa muda wa kurudi tena au utaambiwa kuwa utapigiwa simu japo hutapigiwa, jiongeza baada ya mwezi mmoja au miwili, baada ya kujiongeza ndio hapo usumbufu unaanzia na utapigwa tarehe kila ukionekana. Probability ya kupata hela kwa muda mwafaka ni ndogo sana, itakuchukuwa hadi mwaka mmoja au na zaidi ili kupata hela yako.


Mimi mwenye ni mhanga, niliacha kazi mwezi wa 1, mwezi wa saba nilienda, nikaambiwa mwezi wa 8, nimeenda tena nimeambiwa mwezi wa 12. Kwa kweli ni changamoto mkuu, na hapo natoka Kigoma na ukiangalia madai yangu utashangaa, nafikiri nikisafiri mara 4 hiyo hela itaishia kwenye nauli
 
Kama Una Baba yako, Mama Yako, Bibi Babu, Dada Na Hata wewe Mwenyewe na Wanyonge Wote Serikali ya Awamu ya Tano Imekaribia kuleta Mkong'oto Huu Huu hapa (Kilio na kusaga Meno)

Kuna mswada unakuja na kwa Bunge letu la Wangapi wanakubali Waseme Ndiyooooo "Ndiyoooooo" waliosema ndiyo wameshinda "Utapita"

MSWADA HUO Unaenda kuua wastaafu Na sisi Tunao karibia kustafu

Ni hivi Mafao ya wastafuu yatakuwa hivi Tega sikio, utalazimika kulipwa 38% tu na 62% utakuwa unalipwa kila Mwezi (monthly) hapa ili unielewe nikupe mfano. kama ilikuwa ulipwe milioni 100 kama hela yako ya kustafia maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi.

Ukistafu na umri wa miaka 61 utakula hicho kiasi cha million 38 kigingine utalipwa kidogo kidogo kila mwezi

Ubaya wa hili siku ukifa tu kila kitu kimekufa malipo kila mwezi nayo yanakufa. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma wakati ungepewa yote ungewaachia miradi familia wakaishi hata kama haupo

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu. Yaani LPF, NSSF PPF sijui nani sijui nani itafungwa na kubaki mifuko miwili tu (Vibarua vinaenda kuota nyasi)

4. April 2018 sheria itaanza kutumika Yaani Mwakani Kuna kilio kikuu kwa watumishi wa mifugo na wastafuu

My Take

Kwa ufupi bila kupindisha muswada huu utaumiza watumishi wote ,Bunge Mkafanye kazi yenu, sasa Hiki ni kipimo chenu cha kudhibitisha Mpo huru na kwamba ni muhimili unajitegemea ,Wabunge wetu msipoliona hili kuwasemea watumishi basi Mtawasononesha watumishi

Yaani Ufanye kazi miaka 61 ukitumikia umma uzeeni uporwe haki itasikitisha

Alloyce Nyanda
Mtozi.
 
Back
Top Bottom