Fao maalum la Mkupuo la NSSF (Special Lumpsum Benefit)

A.MTALE

Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
43
Reaction score
18
Wanajamvi Habarini za wakati huu.

Napenda kufahamishwa kwa ajili ya ufahamu wangu na wengineo. Je kama umefungua madai NSSF ya special lumpsum benefit na status ikawa Approved na pia ukiangalia kwenye member's portal kwenye account yangu naona salio ni Zero na contributions zero na number of credits zero je hali ya namna hiyo inamaanisha nini na mfumo wa malipo unakuaje hapo

Ahsanteni sana.
 
Waulize nssf mkuu
Huku unaweza usipate jibu sahihi
 
Hapo maana yake wameshatoa deposit cheque kwenda kwenye akaunti yako mkuu. Mzigo utasoma kwenye akaunti yako ndani ya masaa 72, jiandae kupokea mzigo huo mkuu kwa kishindo na kuweka heshima baa! Hongera.
 
wengi wanadai ikiwa hivyo maanake ni kwamba pesa zipo kwenye mchakato kuingizwa kwenye acc yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…