Wakuu Habarini za Siku ya Leo? Natumaini mu wazima wa Afya. Na wale wagonjwa nawaombea uponaji wa mapema ili waendelee na majukumu yao ya kila siku.
Niende kwenye hoja.
Mimi sikuwa mdau wa kukopa kopa simu ila, baada ya kuwa na kazi kadhaa zinazotumia charge ya simu kwa kasi na kumaliza charge ndani ya masaa 12, nikajaribu kutafuta power bank nikaona nyingi ni fake, nikaamua kudondokea kwenye Samsung A 07 ya mkopo.
Sasa kitu kinachonishtua kwenye hii Samsung a07, ni kwamba, kila baada ya dakika kadhaa, ishara/notification ya kuonesha kuwa camera inatumika inaonekana kwenye screen kisha ina dissappear. Sasa wasiwasi wangu ni je, ina maana kila baada ya dakika kadhaa hawa wakopeshaji wanapiga picha za mahali simu ilipo? Na kama ni hivyo, je huko sio kuingilia faragha ya mtumiaji/mteja kinyume kabisa na sheria za nchi yetu?
Naomba kuwasilisha.
Steve,mara ingine uliza hivi:Kwa nini simu za mkopo hujiwasha kamera mara kwa mara ili Lavit asikupige dongo.Acha kusingizia power bank fake, wewe ni pangu pakavu…kwani hizo simu haziuzwi kwa cash?
HahahaAcha kusingizia power bank fake, wewe ni pangu pakavu…kwani hizo simu haziuzwi kwa cash?
Ninauza simu za mkopo.Acha kusingizia power bank fake, wewe ni pangu pakavu…kwani hizo simu haziuzwi kwa cash?
Haitumiki muda wote. Kila baada ya dakika kadhaa inatuma notification ya kijani yenye alama ya camera kwa sekunde chache kisha notification hiyo inazima. Ni kama vile inatuma picha chap inazima.inaonekana kamera inatumika muda wote sidhani kama chaji itakaa.
Nilimaanisha kuna app ina access na camera muda woteHaitumiki muda wote. Kila baada ya dakika kadhaa inatuma notification ya kijani yenye alama ya camera kwa sekunde chache kisha notification hiyo inazima. Ni kama vile inatuma picha chap inazima.
Nimeamua kuziba camera na tape.Nilimaanisha kuna app ina access na camera muda wote