Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
Mnakumbuka kuhusu hafla ya kumzika malikia Elizabeth ll yalifanyika kwa faragha siku ya mwisho ya kuuweka mwili wake eneo la mapumziko?.
Sasa bwana jambo lile lilizua mjadala huko Uingereza, hoja nyingi zikajadiliwa kwanini walifanya fargha? Na utamaduni wao wamekuwa wakiona tukio la mwisho la kupumzishwa wafalme wao.
Kufatia hilo, gazeti la Times limeamua kutoa ufafanuzi wa jambo lile, kuhusu kile kilichotokea wakati wa hafla ya faragha siku ya Jumatatu baada ya kamera kuzimwa.
Ni kwamba, tukio lile lilifanyika kwa kufuata itifaki mpya ya mazishi yale, itifaki ile ilikuwa inavunja utamaduni wa miaka yote katika mila ya mazishi ya wafalme wa Uingereza, Najua ujanielewa!.
Ni hivi...
Mamlaka ziliondoa kamera kwasababu mazishi ya Malkia yalikuwa yanafanyika tofauti na utamaduni wao huko nyuma, sasa kuondoa taharuki hiyo ikapendelewa kamera kuzimwa na kuruhusu wanafamilia wachache kuhudhuria tukio hilo.
Ni Kwanini hilo?
Ni kwasababu kuna itifaki mpya zilianzishwa kufatia wosia wa malikia Elizabeth ll, sehemu ya wosia huo ulitaka kufanyika marekebisho ya baadhi ya tamaduni ya maziko baada ya yeye kufa.
Kilichofanyika.
Ndani ya kanisa la mtakatifu George kuna chumba kidogo chini ya kanisa hilo yani underground, kwenye chumba hicho kuna eneo maalumu la maziko, hapo ndipo alipo zikwa mfalme George VI na mama yake Elizabeth ll yani queen Mother.
Eneo hilo utaratibu wa maziko upo kwa mtindo wa vault (kuba), sasa upande wa kulia kuna sehemu iliyo pewa jina la "North Quire Aisle", hapo ndipo lilipo kaburi la pamoja ambapo ndani yake amezikwa malikia Elizabeth ll.
Ndani ya kaburi hilo kuna mwili wa mfalme George VI, Elizabeth the queen Mother, malikia Elizabeth ll, Prince Philip na Princess Margaret, Countess of Snowdon.
Sasa mpangilio wa mazishi ni kwamba upande wa kulia kuna jeneza la Mfalme George VI kwa juu na mama wa Malkia Elizabeth kwa chini.
Kushoto kuna jeneza la Prince Philip lilowekwa chini, kisha la Malkia likawekwa kwa juu yake, alafu kwa mbele ya majeneza yote maNne kuna Majivu ya dada wa Malkia Princess Margaret, ambayo box lake lime hifadhiwa kwenye eneo dogo la mbele.
Ni Kwanini hivyo?
Kama nilivyo sema awali kuwa utaratibu huo ulipendekezwa na malikia Elizabeth ll kabla ya kifo chake, malikia Elizabeth ll alipenda atakapo kufa azikwe karibu na baba yake, mama yake, mume wake na dada yake katika kaburi moja kwa mfatano wa itifaki (yani wakae kwenye shimo moja).
Kama malikia Elizabeth ll asinge acha wosia huo, basi yeye na mumewe tu wangezikwa peke yao bila kuambatanishwa na baba yake na mama yake kwenye kaburi la pamoja, badala yake malikia Elizabeth ll na mumewe Prince Philip wangewekwa kwenye vault yao.
Kwasababu ya Code of precedence mtawala lazima awe na shimo la kabuli lake au eneo lake la pekee bila kuchangamana na mfalme mwengine, sasa hii mila ikavunjwa kwa maziko ya Malikia Elizabeth ll kwa mara ya kwanza toka mwaka 1290, toka pale Mazishi ya ufalme yalipo anza kufanyika katika kasri la Windsor.
Utaratibu wa awali wa mazishi ulianza toka kwa Mfalme Edward lll, mpaka ulipokuja kubadilishwa katika mazishi ya Malikia Elizabeth ll.
Kwa kutambua hilo, utaratibu huo ulitekelezwa vyema.
[emoji419]Tazama picha hapo chini kuona namna ilivyo.
Ndimi Comred Mbwana Allyamtu CMCA.