Farhan Kihamu ana majibu yako wewe mfia timu

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Huwa nikisikia Shabiki kwenye Kipaza sauti anaanza kwa kusema “Tunaoumia ni sisi Mashabiki kuliko wao” basi naachana na kusikiliza naendelea na mambo mengine, kwenye huu mpira wetu wa Bongo hakuna Shabiki wa Simba wala Yanga anayeumia kuliko Matajiri wanaoweka mzigo wao kwenye hizi timu.

Yaani uumie kuliko MO na GSM? Unafahamu mechi zote za Afrika wanasafirisha timu kwa gharama zao? Kwakuwa pesa ya mashindano hutoka baada ya msimu kuisha na haiendani na gharama mnazotumia, unaona raha tu kuona Simba wanaconnect flight Dubai, mara Yanga wamelala Istanbul, Wajomba hapo Matajiri wanatoboka na bado hawajalipa posho na mishahara, bado motisha.

Unaumia kuliko Viongozi wa timu ambao wanapambana kusaka Wachezaji Afrika ambao wanakuja kubebwa na wakubwa kwasababu ya pesa? Fikiria Fiston Mayele wale Yanga wanastruggle mpaka leo watu walikuja wakaweka pesa wakasepa nae, Mbwana Samatta mbichi kabisa Simba hajamfaidi sana kasepa Mazembe, unafikiria kuna raha ya project kufia kati kwa Viongozi?

Shabiki uumie kuliko Matajiri? Kwa hoja ipi? Wewe ambaye hela unayo ila Kadi hutaki kulipia, jezi hutaki kununua unasubiri discount? Yaani tujadili kidogo, Al Ahly mwenzako Shabiki wake ananunua pea ya socks kwa 70,000/= ambapo ni sawa na jezi mbili za Simba na Yanga, mwenzako analipa ada ya Uanachama kwa package, Wanafunzi, Watoto, Wafanyabiashara, huyu asemaje kama wewe unasema unaumia.

Shabiki unasema unaumia kuliko Viongozi? Watu wanaenda kupambana na Al Ahly mwenye privaje jet yaani anauliza location mechi ni wapi, anaomba kibali cha anga anatua anapiga mechi usiku anatekenya ndege yake anasepa zake, unafahamu kuwa kila mechi ya Champions League wachezaji wa Simba na Yanga wanachukua bonus mpaka MILLION TANO kwa Mchezaji mmoja tu?

Unaumiaje? Unaumia wakati kwenda uwanjani mpaka ufatwe mtaani na Kispika cha Ahmed Ally? Mpaka Ally Kamwe afanye press mia mia ndio muende? Unaumia wakati Simba App na Yanga App huna, kadi huna, jezi huna, Youtube hujasubscribe? Halafu ghafla unataka timu zikapigane vita kubwa ya usajili?

Mara utasikia watuachie timu zetu! Haya mlifanya nini mlivyokuwa nazo? Simba ya usafiri wa Coaster na mazoezi Kinesi? Yanga ya bakuli na mtia saini ni Ajibu?

Farhanjr[emoji109]
 
Anayeumia ni tajiri wa Azam, yeye kutengeneza timu na anahudumia na uwanja kajenga na Hana mashabiki wa kumsapoti. Hao GSM sijui mo wote wapo kibiashara kwani wamekuta Simba na yanga Zina umaarufu wao na tayari walishapita matajiri wengi na hata wao walipndoka hizo timu zitaendelea kuwepo.
 
Na bado wanapambana kwa Kila hali kumiliki team zinazowapa hasara
Uongo!!!!!!
 
Hakuna timu pasipo mashabiki/wanachama...

Hao matajiri na pesa zao, kama ingekuwa ni kutengeneza timu tu basi wangetengeneza timu za draft au bao ambazo hazihitaji mashabiki...
 
Fikiria Fiston Mayele wale Yanga wanastruggle mpaka leo watu walikuja wakaweka pesa wakasepa nae
 
Ameongea ukweli lakini kwa jicho jingne hasa la kibiashara hakuna tajiri anayeweka pesa yake sehem ambayo atapata hasara na kama wangekuwa wanapata hasara wasingekuwa wanaendelea kufadhili hizi tim
Kwani wewe ukifanya biashara isipokupa faida hapo kwa hapo unaiacha?.Inawezekana wanafaidika indirect kupitia huo ufadhili au malengo yakunufaika kisawasawa niya miaka mingi ijayo.Kama mtu umeshaweka mtaji na faida haionekani na pesa haijarudi ila ukiangalia kuna uwezekano wakupiga ela uko mbele unakomaa tu kwa matarajio fulani sio kukimbia alafu mtaji ufie chini.
 
Kaandika udwanzi [emoji16]
Je hao matajiri wanapata faida kiasi gani kupitia brand za hizo timu??
 
True
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…